Saturday, May 22, 2010

Swali:- Mmmea huu una sumu au ni uzushi?

Nimeletewa ujumbe huu jana na dada Penina kwa kuwa hili ua ni hatari na nimeona niweke hapa ili kufikisha ujumbe huu na kwa wenzangu.

Upo ujumbe unaozunguka katika barua Pepe ukifahamisha Rangi kuwatahadharisha Watu kuhusiana Rangi mmea ambao wengi wetu tunaufahamu kama Ua ama pambo la nyumbani. Ujumbe umeandikwa Kwa lugha ya Kiingereza lakini mdau Ray Njau ameutafsiri Kwa lugha ya Kiswahili mama ambao unasomeka hivi:

Unaoonekana pichani mmea unapatikana Kwa wingi nchini Cameroon (Hata hapa Tanzania), ofisini, majumbani Rangi kwenye bustani, Ni sumu hasa Kwa Watoto, unaweza kumuua Mtoto ndani ya dakika 15 baada ya kuweka Tu kinywani. Ukigusa huweza kusababisha upofu macho "Wa kudumu.

Swali: Je Habari Hii INA UKWELI WOWOTE AU Ni ya UDANGANYAFU Tu?

5 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Ooops! ngoja nikimbie nyumbani nione kama upo nikautoe...:-(

Duh!

Anonymous said...

Da Yasinta, inaelekea aliyekutumia ujumbe huo alitafsiri (au alipokea tafsiri) kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili kwa kutumia Google Translator (mashine) na hivyo kukosea mtiririko ulio sawa (nimecheka nilipokuwa nasoma hiyo tafsiri).

Hata na hivyo, ujumbe huu niliwahi kuupokea kwa lugha ya Kiingereza na kuupokea kutoka kwa bw. Ray Njau aliyeutafsiri kwa lugha ya Kiswahili na kutaka wadau wachangie maoni yao, na wapo waliochangia kama inavyoonekana kwenye posti iliyopo hapa (bofya).

José Ramón said...

Una blog ya kuvutia sana.

Salamu kutoka kwa ubunifu na photos mawazo ya José Ramón

Penina Simon said...

Ha ha ha,

Mimi kwa upande wangu naweza amini 50%, kabla hata ya mimi kuipata hii, binafsi nalipenda sana hili ua jinsi lilivyo linanivutia sana na hasa likikubali mbolea halafu halina tatizo la ukuaji,
nimekuwa nikiyapanda sana nyumbani kwangu, siku moja niliona ua limekua sana na kuzaa hadi limejaa ndoo, nikaona nilipunguze na kuliotesha kwingine pia, sikuwa na vifaa vya bustani hivyo nilitumia mikono, loh!!!!!!!!!!! maji yake yaliponiingia mikononi niliwashwa hadi nilikoma, manake siwezi kusema ni muwasho, nilikuwa nahisi kama mikono inawaka moto, nilinawa sana haikusaidia hadi ilipokoma yenyewe mikono ikawiva kama nimepitiwa na moto.Hivyo kwa maana hiyo nahisi kama ukijisahau ukashika jicho, utaimba pambio zote na kutubu madhambi yako yote (i mean utakoma kama siyo kupofuka)

Bennet said...

Huu mmea unaitwa dieffenbachia na mwingine jamii ya cladium yote tunaitumia kama maua majumbani kwetu, hii mimea ina sumu lakini haijafikia kuua, kwa mfano ikitafunwa utawashwa mdomo na utavimba kiasi lakini baada ya muda utarudi kwenye hali yake ya kawaida na hata ukijipaka kwenye ngozi pia itaathirika kwa muda lakini utapona bila kutumia dawa

kwa kifupi ni kwamba kuna vyakula vyenye sumu mfano mihogo na viazi pia vina sumu ingawa ni kidogo sana kiasi amabcho huwezi hata kuhisi