Monday, May 16, 2011

OMBENI NANYI MTAPEWA!!!!!

Fataki kampa lifti dada mmoja aliyekuwa akitoka kanisani. Kwa kuwa dada kabeba biblia Fataki akajua dada huyo ameokoka. Ndani ya gari Fataki kila akibadili gear anashika mapaja ya dada. Dada akamwambia kasome Mathayo 7.7. Fataki akajua amelaaniwa na hata alipomfikisha dada anapokwenda hakuomba namba yake ya simu. Fataki kufika nyumbani akasoma andiko kwenye biblia akapiga kelele, Duh! Nimekosa kijinga, maana andiko linasema OMBENI NANYI MTAPEWA!!

Ebu tuangalie na hapa....

11 comments:

Simon Kitururu said...

:-)

Anonymous said...

Da, Yasinta,neno la mungu nilaajabu kwelikweli na linanguvu sana tena sana.Fataki alikuwa nanguvu za shetani, ndomaana hakuwa na ufahamu wa kile kilcho nenwa na yule dada. mungu alikuwa upande wa yule dada,fataki alikuwa yeye kama yeye binaadamu wakawaida mwenye kutumainia tamaa bila kumtanguliza mungu mbele katika kila jambo.kwangu mimi neno kuomba lina maana sana,na kuomba si mchezo inahitaji ujasiri wa haliya juu. kaka s

Christian Sikapundwa said...

NAKWITA Mwana- Saikolojia,Dada Yasinta,pamoja na maneno matakatifu kwenye maandiko,hayafui mwingii mwenye tamaa za kishetani.Zitampeleka kuomba hata pasipo ombeka kisha anajilaumu Nasfi yake wakatu huo shetani yuko kando akimwangalia tu uwezo wa kumtoa hatakuwa nao aslani.
Hawa mafataki hawaogopi Biblia au maombezi wao ni kutimiza ufataki wao muda wowote,rika lolote eneo lolote,kutokana na sifa za ufataki,mtu kama hana sifa hizo huyo si fataki atakuwa baruti.

Mwanasosholojia said...

Shukrani kwa ujumbe maridhawa Da'Yasinta. Haya ni mambo tuliyonayo katika jamii yetu inayotuzunguka. Tuna kazi ya kupashana habari, kuelimishana na kuonyana. Umeifanya kazi hii, tuna wajibu wa kusaidia kuisambaza kwa wengine. Siku njema kwako!

emu-three said...

Ujumbe safi sana wa kiimani, shukurani dada yetu Yasinta, kwa ujumbe huu!

Salehe Msanda said...

Duh,
Hapo hata huyo dada alitakiwa kujua kuwa kuna lugha nyingi za kufikisha ujumbe na ndo maana baada ya huyo dada kugundua hilo akamwambia fataki akasome hicho kifungu. Lakini inaelekea dada aligundua hiyo lugha ya ishara akahitaji kutamkiwa kwa maneno.

Unadhani ingekuwaje iwapo huyo fataki angekuwa anafahamu hicho kifungu kinasema nn.
Hiyo changamoto inanikumbusha maandiko ya Munga katika moja ya makala zake katika lililokuwa gazeti la jitambue iliyokuwa inasema kama sikosei biblia au yesu aliupendelea ubepari/mabepari katika kifungua kile alichosema aliyenacho ataongezewa.

Kwa tafsiri ya kimafanikio kifungu hicho kinamaanisha kama utafanya juhudi katika suala fulani kwa nia njema utapata kile unachohitaji zaidi na zaidi. Badala yake tulio wengi badala ya kufanya juhudi za kuongeza tunafanya juhudi za kupunguza hata kile tulichonacho. Mfano mdogo wengi wa watanzania tuna tatizo la kutokutunza akiba tukisubili kupata kingi ndipo tuweke akiba(saving) wakati matajiri wao kila siku wanahakikisha kile wanachokipata wanaweka benki na kuwekeza katika mradi wa kuongeza kipato. Na ndio maana wanazidi kupata zaidi na zaidi.

chib said...

Huyo Dada aiache hiyo Biblia kabisa, maana kupewa lifti na mtu anyeonekana kashetani naye anamfungulia mlango kwa ishara. Wote na Fataki wanahitaji kuombewa sana!

Simon Kitururu said...

Huyu dada nafikiri naye alihitaji kujifunza kukubali sio kimafumbo.

Jibu lake la mpaka kwenye biblia la ``OMBENI NANYO MTAPEWA´´ kama maana yake ilikuwa kama MKAKA angemuomba tu angekubali,...
.... labda naye alikuwa anahamu ya kitendo alichostukia FATAKI anataka kufanya naye kwa hiyo angekubali tu kwa sentensi za kawaida FATAKI na YEYE wote wangewini kufanikisha hiyo dhambi.

Tukiachana na FATAKI na huyo mdada na kurudi tu mtaani ,...
.... WANAUME na WANAWAKE kimatumizi ya lugha hasa wakati wa kutakana huchanganya sana. Ni rahisi MKAKA wakati anafukuzia kudhania hapendwi na huyo MDADA amfukuziaye kisa LUGHA. Unaweza kukuta MDADA kumbe naye anataka lakini kuanzia lugha ya mwili aka BODY language na kauli aziongeazo unaweza kudhani unanyimwa kumbe wala. Mpaka mtu unaweza kukata tamaa halafu unasikia labda kutoka kwa marafiki zake mrembo kuwa anakuhusudu kweli na unaanza kujiuliza sasa mbona ukiongea naye hakieleweki.:-(

Lugha hapo juu kwa mtazamo wangu ndio tatizo ingawa nashamngaa kwa kusoma maoni ya watu hapa kuwa wengi wanapata funzo la KIIMANI wakati mimi niliona huyo mdada ni wale tu wa UNIANGUSAGE! Si nasikia kuna WADADA ambao kamwe hawawezi kukubalia mwanaume kwa sababu za kimili na ni mpaka waanguswage tu?.... ingawa hili jambo nasikia linatumika sana na VIDUME kuhalalisha kubaka wadada za watu kisa ingawa mdada katoa nje kikweli VIDUME wanajiaminisha anataka ila anasubiria ili ukiona kaanza kulewa umuangusage tu!

NI wazo tu hili !

Koero Mkundi said...

Kaka Kitururu, wakati mwingine kugaiwa kiulaini huwa hainogagi....
Kwa kule vijijini kutokana na ufinyu wa tamathali na mbinu za kukatalia kidude huwa mbinu ya niangusage au chagulaga inatumika sana....
Kwa huku mijini, tumesoma na tunaishi kizungu, hizo mbilinge za niangusage, hazina nafasi, wanaume wa mijini wana deka sana, kwanza wala chipsi mayai watakuwa na nguvu hizo? Midume iko vijijini, humpati mwanamke mpaka mpigane mieleka.... hakuna kula bila jasho.

sasa nikirejea kwenye mada, ni kweli watoa maoni wengi hapa wanajaribu kupotosha ili kufanya mdada aonekane alikuwa na imani hasa, kumbe ndio wale wale wa niangusage ki-mjini mjini, hana lolote, Fataki angelijua neno angekula kiulainiiiii.

Kaka Kitururu, enzi za kuzungushana hazipo siku hizi, Kujifanya unapanga mashairi ya kutongozea ni kupoteza muda, wenyewe siku hizi tunakwambia...... acha Longo Longo, we sema una sh.ngapi?

Umekaa sana huko ughaibuni na ndio maana haya huyafahamu...LOL

Rachel Siwa said...

Asante sana da Yasinta kwa ujumbe mzuri!!!@kaka Kitururu wewe umesikia wapi hiyo NIANGUSAGE?Kwikwikwikwi

Simon Kitururu said...

@Rachel: Sitanii nilishawahi kuambiwa hicho kitu na Mdada mmoja wakati mwenyewe nabembeleza!

Halafu napenda kweli kicheko chako cha ``Kwi kwi kwi!´´:-)