....nikaikatatakata kama muonavyo katika picha , wakati huo nishaweka maji katika sufuria ...
...ipo ndani ya sufuria ili ishemshwe kwa muda wa dadika 2-5
na hapa baada ya dakika 2-5 inaonekana hivi, baada ya hapa nasubiri ipoe na halafu
...naiweka katika mifuko kwa ajili ya akiba na pia naandika tarehe na ni mboga aina gani, baada ya hapo ni kuweka kwenye friza(freeze) ...mjanja eehhh:-)
13 comments:
Yaani mjanja mnoooo...dah nimetamani dada uwiii....kwenye friji zitakaa kwa muda gani? hongera sana kwa kulima
Mama A! ahsante kupita hapa na kuacha yako ya moyoni...Kwenye deep frriza itakaa hata miaka ndugu yangu:-)
Hongera sana Kadala..Mhhh nimeitamani sana....
oooh asante sana dada kwa maujuzi......
Dada yangu umenitamanisha na mboga ya maboga.Naomba kuuliza je naweza kuifadhi mboga ya mchicha kwa njia hii??Asante
Manka ndugu yangu haswaaa unaweza hata kusamvu pia tembile na kadhalika. Nilikumissije!!!
Yay..asante sana nitafanya hivyo.Nami nilikumisi Dada yangu
Habari yako Dada Yasinta.naomba kukuuliza kwani kuna mbegu za kuvuna majani ya maboga tuu bila kuota maboga.au ni yale yale ya maboga ndio mnavuna majani yake. msinicheke jamani nataka kujua na tena ni mgeni humu.
Mama wane.
ndugu yangu mama wane...kuuliza si ujinga. Hizi mbegu nilipewa na mama yangu wa hiari Njombe ni mbegu nyeusi mara nyingi hustawi na kuvumilia hali ya hewa ya ubaridi kama ile ya Njombe, Iringa, Makambako na pia niliishi Madaba_Matetereka. Huwa hayawi mabogo ni mboga tu. Na zile mbegu zitoazo mabogo hapa hazistawi sana hii ndiyo sababu kubwa.
ahsante dada yasinta kwa kunijulisha.samahani nimechelewa kushukuru watoto walinipelekesha kidogo.Mimi nipo Canada ,naona hizo mbegu zitanifaa.nitaziagiza Dar kama zipo.
Mama Wane.
Mama Wane....Unaweza kuniagiza nitakwenda nyumbani karibuni ukitaka.. ..si unajua maisha kusaidiana...
nimeitamanije na hasa inavyopikwa kiusafi
Kaka Mwangoka! Usitamani tu Karibu nimekuwekea!
Post a Comment