Saturday, October 3, 2009

MUHIMU: CHUNGUZA KWA MAKINI KWANZA!!

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.

Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.
Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi (authentic) na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.
Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja (mtanashati) alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.
Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!
Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).
Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja. Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia (hearing aid). Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa, Guess what!
Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!
Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!
Chanzo: The Hill Of Wealth

16 comments:

Unknown said...

Ha, ha ha ha haaaaaaa.....kwi kwi kwi kwiiiiii!!!! Duh!!!!
dada umeitengeneza sku yangu ya leo....kaaaaaazi kweli kweli....

Kweli chunguza kwa makini.....LOL

Albert Kissima said...

Haraka haraka haina baraka,
Polepole ndio mwendo,

pia,

usione kinang'aa ukathema ni zaabu,

Vijanaaaa! Nashema vijanaa!
Hii n'shomo zui kwei kwei,

Bennet said...

Kuna wengine wanakuwa na tabia bandia yaani wakati wa uchumba anaficha makucha yake (mme/mke) lakini akiingia kwenye ndoa ndio anabadilika na kuwa halisi

Unknown said...

Yaani nimesoma nikabaki kuduwaa, i can imagine huyo kaka wa watu alipata mshtuko wa ghafla..da kweli ni muhimu kuchunguza hivi vitu..
Pole pole ndio mwendo na harakaharaka haina baraka...

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta nimeshusha pumzi kwa nguvu nilipomaliza kusoma. Bonge la fundisho.

Koero Mkundi said...

Ni kweli dada kuna haja ya kuchunguza maan siku hizi mhh!!!
yataka tafakuri....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

inaonekana yule kijana alipenda sana mambo ya bandia. lakini bado si ni mtu na kile alichotaka kukioa yaani uke, si kilikuwepo? aoe tu

Chacha Wambura said...

KL, alichokitaka ndo kilimfanya azimie kwani angeoa mke a.k.a uke asingestuka na kuzimia.

kuna baadhi yetu tunaoa/olewa na sauti, kucha, nyusi, bambataa, guuguu, gadelavu nk nk na ndo matokeo yake kama hayo ambapo tunapata msituk kukuta mume/mke kikojozi, mmbeya ama mdokoa finyango chunguni...lol!

John Mwaipopo said...

hivi ukitaka kununua gari huruhusiwi kuliendesha japo kilomita mbili hivi?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mwaipopoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

tehe tehe teheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

chib said...

Piga ua, kuna watu hawabadiliki na vitu vya bei poa, hata kama uwezo wanao, ni kama jadi vile

Yasinta Ngonyani said...

Yote mmmesema lakini si mbaya kurudia ni kweli kuchunguza ni muhimu lakini wengine mnachunguzana na na kila kitu kinakuwa safi na ndoa iksha kuwa tayari zile tabia mbaya zinaanza kujionyesha. Cha msingi ni kwamba hakuna binadamu aliye BORA zaidi kulika mwingine kila mtu ana kazoro yake. Ni hayo tu karibuni tena hapa kibarazani MAISHA.

NURU THE LIGHT said...

ndio maana napendaga nikiingia hapa huwa napata somo la maisha...hii stori ni nzuri sana na inaelimisha mambo mengi,,

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli Nuru ni somo nzuri sana!

Anonymous said...

Ηello, і read your blog frоm time to tіme and i own a simіlar οne and i was ϳust wοndеring if you get
a lot of spam comments? If so how do yοu reducе
it, any plugin οr anything you саn advise?
I get so much lately it's driving me crazy so any assistance is very much appreciated.

My page Payday Loans Online
my web page - Payday Loans Online

Anonymous said...

They have probably not applied credit holders this is usually burdensome, particularly if you are just generating
it without room for extras within the spending budget!
Breaks an online lender can spite of having bad
payday lenders that provide various amounts? Under this scheme you are not required to
perform any kind of formalities or mail, offering them as an easy way to get your hands on big lump sum.
If you have any queries about overnight with also loans
valuable for its easy application method.

Also visit my weblog - Payday Loans - -