Tuesday, March 20, 2012

UMEWAHI KUFIKIRI KUWA HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUPOTEZA MAWASILIANO NA RAFIKI, MPENZI, MUME/MKE AU LABDA NISEME JAMII KWA UJUMLA?

Basi mwenzenu yamenikuta nimempoteza rafiki yangu mpenzi . Namtafuta kwa kila hali na mali lakini simpati. Na jinsi ukimya uzidivyo nazidi kukosa raha. NAMPENDA SANA RAFIKI YANGU HUYU. KAMA UMESOMA UJUMBE HUU TAFADHALI NTAFUTE SITAKI KUKUPOTEZA.....Dada Yasinta nifanye nini ili rafiki yangu aongee tena nami?
-------------------------------------------------------------------------------------------------Ujumbe huu nimetumiwa na mdau ambaye ni msomaji wa Maisha na Mafanikio...nikaona niweke hapa ili mnisaidie ni ushauri gani kumpa mwenzetu.

11 comments:

ray njau said...

Haya wadau wa kibarazani ujumbe ndiyo huo.

Anonymous said...

kweli kumpoteza rafiki nishida sana ila mimi tulipotezana narafiki yangu miaka 25 iliyopita ninaishukuru facebook tumewasiliana juzi.....

Rafikio wa Hiari said...

Naomba nitoke nje ya mada kidogo: Rafiki yangu wa hiari naogopa nisije kupoteza na wewe bure! Maana tumekua kimya kimawasiliano - ninauguza mwenzio. Nitakutumia sms kukujuza zaidi. Naomba nitumie nafasi hii kukwambia nakupenda na kukuheshimu rafiki yangu wa hiari!

Simon Kitururu said...

Na marafiki tuwatunze moyoni na sio kwenye pete kama WAKE/WAUME kwenye ndoa za kisasa!

Yasinta Ngonyani said...

Ray tupo pamoja hata wewe unaweza kusema kitu:-)
Usiye na jina ntamwambia afanye hivyo..Ahsante kwa ushauri..

Rafiki wa Hiari!
Wala usiwe na shaka na pole kwa kuuguza..ntakutafuta pia

Kaka Simon ni kweli inabidi tuwatunze haswa kwani rafiki ni bora kuliko mwanasesele/re..Hii ndio sababu mdau huyu anamtafuta rafiki yake kwa vile yupo moyoni mwake...

Simon Kitururu said...

Nimekuelewa Kadala@Da yasinta

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi kama umenielewa Kadoda...Nawe unamshaurije huyu mdao maana inaonekana anammiss na kumjali kweli rafiki yake mpenzi...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

RAFIKI YANGU NI YESU!!! ASHAONDOKA DUNIANI, KWA HIYO SINA RAFIKI

batamwa said...

mhhh kamala ni kweli????!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kamala! Una uhakika huna rafiki zaidi ya Yesu? tunataka kujua kama kweli upo mpweke kabisa?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nasema harafu hamuamini, semeni wenyewe mtakavyo basi