Monday, March 5, 2012

NINGEPATA MLO KAMA HUU JIONI HII INGEKUWA RAHA ...


Ndizi za kuchoma , ukipata na kachumbali hapa mambo si mabaya nazimezea mate kweli hapa nilipo...au
sijui nikipata hawa senene ila sijawahi kula sijui ni watamu kama kumbikumbi au?
Picha kutoka kwa mwenyekiti Mjengwa.
6 comments:

ray njau said...

Ama kweli mlo huu ni wenye ladha asilia kwa jioni njema itakayohanikizwa na usiku mwanana wenye ndoto njema na usinginzi mnono.

Seleman Awadh said...

umenikumbumbusha vyakula vyetu vya asili ingawa mara tu watu wafikapo mjini huvisahau tena ukimkumbusha anweza vomit!!!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Ray na Seleman...hakuna vyakula vitamu kama vya asili...bahati mbaya sijapata ndizi wala hao senene nimeishia kutamani tu...

batamwa said...

yasinta senene ni watamu kuliko kumbikumbi ingawa wewe umeandika kumbukumbu,dar wanauzwa wengi siku ukija watafute

Yasinta Ngonyani said...

batwamwa! kama ni hivyo nimekosa uhondo...nitafuata ushauri wako...Ahsante nimerekebisha kumbikumbi....

Rachel siwa Isaac said...

Senene sijawahi kula sasa sijui kama nzuri, duuh hapo kwenye ndizi chomaaaa duuhh mamaaaaaaaaa ngoja nikimbie wewe dada ni mchokozi sana tuu!!!!!!!!