Wednesday, August 29, 2012

TANZANIA NI NCHI AMBAYO INA VIVUTIO VINGI AMBAVYO HUWEZI KUVIONA KATIKA SEHEMU YOYOT DUNIANI...!!!

Kama  Olduvai  Gorge Ngorongoro......
 ....au katika mbuga hii ya Serengeti.....
.....na bila kuusahau mlima wetu mtukufu Kilimanjaro
Tumalizia na wimbo huu ....
MUWE NA SIKU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA.....

8 comments:

Interestedtips said...

Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaa....nakupenda kwa moyo woteeeeeeee......kusema ukweli naipenda sana hii nchi, ukiachilia mbali tofauti zooote

Emmanuel Mhagama said...

Ukianzisha habari ya vivutio, huwa najisikia AIBU juu ya jambo moja kubwa. Wageni wa kutoka nje ya nchi hii wanavijua zaidi vivutio vyetu kuliko sisi wenyeji tunavyojua. Licha ya kuwapo hapa Morogoro, mbugani Mikumi zaidi ya kupita wakati naenda kunyumba, nimewahi kwenda kutembea mara moja tu, tena ilikuwa study tour maana nilikuwa shule wakati huo. Kwa mtindo huo hata naona aibu kuviita vivutio maana vingenivutia kweli nadhani habari ingekuwa tofauti.
Sijui nyie wenzangu...

sam mbogo said...

Da Ester,posuta...? nina wiki sasa tangu nirudi kutoka TZ,nimefanikiwa kufika Hifadhi ya katavi pamoja na ziwa katavi. hakika ni mbuga babukubwa . ile mbuga bado (bikira) kuna mandhari safi kabisa kwa utalii mkoa huo mpya unawezakutajirika sana kama watautangaza vizuri. kwa kazi yako Ester unaona sehemu nyingi sana za Tanzania, likizo nimefaidi sana bila kusahau mwanza nipazuri pia natamani kuishi mwanza,tanzania kweli ni nchi nzuri na inavutia,tembea uijuwe TZ.kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Ester! haupo peke yako kwani hata mie naipenda sana TZ yangu na najivuna sana kuwa mTanzania.

Kaka Mhagama! nakuelewa sana na huwa inauma sana kufahamu sisi wenyewe hatujui vivutio hivi...Lakini pia nikuambia kitu kimoja ni kama kawaida tulivyo waTanzania kwenda mbugani kuangalia wanyama au kumnunulia mtoto kitabu hii si mila na desturi yetu anaona ni afadhali aende kilabuni...Watanzania tumejifunga, hatujafunguka, kila kitu kwetu tupo nyuma hatuona wanavyoona wengine...

Kaka Sam!Hongera sana kwa kuwa nyumbani na kuweza kuwa na wakati mzuri wa kuweza kutembelea hiyo mbuga/hifadhi na pia ziwa...na kama bado ni (bikira) basi itabidi tuitangaze...

Anonymous said...

Yasinta, nashukuru leo umetupeleka nyumbani TZ, hakika mie nimejisikia kama nipo TZ kwa kuangalia hizo picha za mbugani na mlima wetu mzuri Kilimanjaro. Kwa kweli pamoja na kuzaliwa TZ sijawahi tembelea mbuga za wanyama hata moja, ni kwa kupita mikumi tu wakati nasafiri. Cha ajabu nilipoenda Switzerland nilienda kwenye Zoo ya wanyama..aah! Sasa
cha ajabu wana wanyama wengine toka tanzania wana majina ya kitanzania kama asha! sasa kumkuta twiga-asha ulaya mh!.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu! Yani hata mwenyewe hapa nimejikuta nipo nyumbani kabisa...Halafu nimecheka kweli hapa Twiga -Asha duh! haya sasa mengine...

ray njau said...

Karibuni Tanzania kwenye ardhi ya mlima Kilimanjaro,visiwa vya Zanzibar,mbuga za Serengeti na kituo cha biashara kwa nchi za eneo la maziwa makuu kupitia bandari ya Dar es salaam.

Justine Magotti said...

kweli siku za mwisho zimefika