Tuesday, August 14, 2012

NIMELIPENDA GAUNI HILI JAMANI..!!

Mdada huyu kila nguo anayoivaa inamkaa utafikiri ndo ilitengenezwa kwa ajili yake..Ingekuwa hivi na kwa sisi wengine ingekuwa bambi kweli..Nimelipenda gauni hili jinsi lilivyo hakuna makolombwezo mengi, rangi nzuri na la heshima yaani ndefu.... Ngoja nitaichukua picha hii nikashone hivyo Je? unafikiri nitapendeza kama mdada huyu?

10 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Kadala ninauhakika itakupendeza zaidi ya huyo dadangu!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! Ahsante kwa kunipa moyo ntashona tu ww ngoja...

ray njau said...

Daima ajaribuye hufanikiwa na muoga katika kujaribu si mdau katika mchakato wa maisha na mafanikio.Acha tuone.................................................................................na tutajua kilifanya sita na tisa zifanane kwa kutofautiana.

EDINA J KIBOMA said...

Hata mimi nimelipenda.
Namuunga mkono huyo alosema utapendeza zaidi hata ya huyu.

Rafikio wa hiari said...

Usitie shaka rafiki yangu utapendeza pia, tena sana tu! Usisahau kutuwekea picha yako

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! ni kweli nikijaribu nitaona uzuri wake...

Dada Edna! kwanza karibu tena. Na halafu nashukuru kwa kuungana nasi..

Rafiki wa hiari! Ahsante sana na wala usikonde nikishona picha lazima muione:-)

ray njau said...

@Yasinta;
Katika chaguo la mitindo ya mavazi kwa wanawake masharti na vigezo kwa maumbile ya mwili huzingatiwa na siyo suala kusema tu mtu atapendeza.
Je wewe maumbile yako asilia yanakidhi vigezo vya vazi husika au kwa ridhaa na shauku ya moyoni umeamua kuulazimisha moyo wako uhisi kuwa hili ndilo chaguo jema??????????

Rachel siwa Isaac said...

Kaka Ray Njau, Yamezingatiwa ndiyo maana mimi na da'Edna Kiboma tukasema itakuwa zaidi ya huyo!!

ray njau said...

Kwa heshima na staha kwenu dada zangu wapendwa nasema:
Acha tuone na kamwe tufikirie kuvuka daraja kabla ya kulifikia.
Salamu!!!

ray njau said...

"Acha tuone na kamwe tusifikirie kuvuka daraja kabla ya kulifikia."