Thursday, September 27, 2012

JINSI YA KUPEANA HABARI KATIKA NDOA ZETU!!!

Tunayo methali isemayo:- "Kisima kikinyauka ndipo tu tunapojua thamani ya maji". Ndivyo ilivyo mara nyingi. Wakati kitu fulani kinapokosekana ndipo tunajua umuhimu wake. Tunapokuwa na afya njema, hatumshukuru Mungu kwa kutujalia afya nzuri na mwili wenye nguvu. Tukipatwa na maradhi ndiyo tunatambua kuwa afya njema ni kitu chenye thamani kubwa. Hali kadhalika, tunashindwa kuwashukuru rafiki zetu kwa ajili ya wema wao kwetu, lakini tukijikuta katika hali ya upweke na huzuni, ndipo twatambua jinsi urafiki ulivyo na thamani sana kwetu.
Ndivyo ilivyo kuhusu kupeana habari. Mara nyingi natambua uhuhimu wa kuongea na mwenzangu wakati ambapo tunakuwa tunakosa kuongea pamoja kwa muda fulani. Ndipo tunatambua kile kinachokosekana, tunaona kila kinachotutenganisha. Hapa tunajaribu kuona jinsi hali inavyokuwa wakati ambapo huna uhusiano mwema katika kupeana habari, na pia mambo gani ya kuhuzunisha hutokea wakati uhusiano unapokuwa si mzuri katika kupeana habari au kutopeana habari kabisa kati ya watu wawili.

Ebu tuangalie mfano huu:- John na maria waliishi katika ndoa kwa muda wa miaka miwili. Walipendana lakinai hakuna aliyemwambia mwenzake juu ya jambo hili. Waliamini ya kwamba kwa kawaida watu wawili waliooana wanapendana, sivyo? Lakini Maria alikuwa na mashaka na Joha. Wakati walikwenda kwenye sherehe au sikukuu fulani, John aliwasifu rafiki zake Maria jinsi walivyokwatua na kuvaa malidadi na jinsi walivyosuka nywele zao. Hata mara moja hakumsifia mkewe au kusema neno lolote la namna hiyo. Maria hakuthubutu kumwambia John juu ya jambo hili. Alizidi kukaa kimya. Siku moja, John alimwuliza Maria, Una nini Maria? Unaonekana huna furaha wakati wote, Hakuna kitu chochote, bali nimechoka tu siku hizi, alijibu Maria.
Kumbe, Maria alikuwa anasema uwongo. Alijua kwamba alikuwa hasemi Ukweli. Lakini John hakujua. Baada ya miezi mitatu kulizuka ugomvi kati ya John na Maria kuhusu fedha, na ndipo ukweli ukaonekana. Kwa kweli Maria hakugombana kwa ajili ya fedha hata kidogo ilikuwa tu ni kisingizio kilichotafutwa ili kuanzisha maneno makali. Sababu ya kweli ilikuwa kwamba Maria alihisi kwamba John alikuwa hampendi tena bali mapendo yake yalielekea kwa wanawake wengine. Kitu kidogo; yaani, kuacha kumsifia na kumwonea fahari mkewe ampendaye kweli, sasa kimekuwa kitu kikubwa, yaani Maria amekuwa na mashaka juu ya mapendo ya mumewe kwake. Kupeana habari kati yao kumekosekana na kitendo hiki kikikomaa, mambo madogo hugeuka kuwa makubwa.
chanzo: KITABU CHA NJIA YETU KWA MAPENDO NA NDOA.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ujumbe wangu ni kwamba katika ndoa tuwa na MAWASILIANO NI MUHIMU SANA.

7 comments:

Emmanuel Mhagama said...

No comment.
Message sent, delivered and read. Mwenye masikio na asikie neno hili.

SIKU NJEMA WAPENDWA.

Anonymous said...

Kumbe wanaume wengi wanakosea bila kujua na pengine si kwa nia mbaya ila tu basi. Kazi ya mungu haina makosa aliumba binadamu na kupandikiza wivu na upendo hatuna budi kuwa makini sana na Ndoa zetu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama! uwe salama nawe pia!
Kaka Goodluck!Sio wanaume tu wanaokosea hata wanawake wanakosea hapo inawezekana kwamba Maria naye hana mazoea ya kumwambia John hayo maneno na alisema makusudi kwa rafiki zake. Na ndio maana mawasiliano ni muhimu sana si katika ndoa tu bali kwa ujumla yaani kusema lile linalosusibu ndani ya moyo wako...kuwa mkweli. Kwa sababu usiposema inakuwa hivyo kumwelewa mwingine tofauti. TUWASILIANE MARA KWA MARA.

Rachel siwa Isaac said...

Asante kwa ujumbe da'Kadala.......

EDNA said...

Asante kwa darasa mdada.

Anonymous said...

yaani hii ni ajabu na kweli hii sentensi ya kwanza nilipoanza kuisoma utafikiri nimeandikiwa mm kabisaa maana nipo ktk situation hiyo kwa ss duh mpaka nimeogopa

gadiel mgonja said...

Ahsante dadaa kwa ya leo,nikweli john alifanya kikosa kidogo ila maria nae hakuwa muungwana kwani amelichukulia kubwa na kua mkimya kwa john,john ni mumewe hivyo kwa swala kama hilo taratibu na kwa unyenyekevu angemwambia john kwamba hujantendea haki baba na john labda angemweleza vizuri tu sabuba ya kuwasifia rafiki zake na angejua nia yake kuliko alivyofikiriakua mzee atakua amewapenda kimapenzi,hayo yote n kutoamiana laiti kama angekua anamuamini mzee wake asingewaza hayo ambayo anayawaza na yanamuumiza kichwa na baadae kuifanya ndoa iwe ya karaha,ila tushawazoea wanawake walivyo ni kuishi nao kwa akili tu,kama kwa wale tunaosoma na kuiamini bibilia tunaambiwa kua wanawake ni viongo dhaifu hivyo tuishi nao kwa akili.jion njema.