Monday, September 3, 2012

TANZANIA YANGU NA MAKABILA YAKE NA UTAMADUNI WAKE..WAGOGO TOKA DODOMA.!!!

Tanzania ni nchi ambaye ina makabila mengi sana zaidi ya 130..Na kila kabila lina mila na utamaduni wake. Binafsi najivuna sana kuwa mtanzania leo tuwatembelee wenzetu wagogo kwa mtindo wa kuwasikiliza wakiwa wakiimba na kucheza..

JUMATATU NJEMA KWA WOTE....

3 comments:

ray njau said...



UNAPOTAJA JINA KILIMANJARO KWA HAKIKA UNATAJA TANZANIA KUTOKANA NA UMAARUFU WA MLIMA KILIMANJARO AMBAO NI MAARUFU KULIKO YOTE AFRIKA.NGOMA KUBWA YA ASILI YA WACHAGGA NI IRINGI. IRINGI HUCHEZWA KATIKA MDUARA HUKU WATU WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO IKIWA NI ALAMA YA UPENDO NA MSHIKAMANO WA KIFAMILIA .ZAO KUU LA BIASHARA NA UCHUMI KWA WACHAGGA NI KAHAWA CHINI YA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA [KNCU].WACHAGGA WANAISHI KWENYE WILAYA NNE ZA MKOA WA KILIMANJARO AMBAZO NI SIHA;HAI;MOSHI NA ROMBO KWA MPANGILIO UFUATAO:

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

1.WASIHA

2.WAMACHAME [ WILAYA YA SIHA NA HAI]

3.WAMASAMA

--------------------------------------------------------------------------------------------------------

4.WAKINDI

5.WAKIBOSHO

6.WAURU

7.WAOLDMOSHI

8.WAMBOKOMU [ WILAYA YA MOSHI ]

9.WAKIRUA

10.WAKILEMA

11.WAMARANGU

12.WAMAMBA

13.WAMWIKA

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

14.WAKENI

15.WAMKUU

16.WAMASHATI [ WILAYA YA ROMBO ]

17.WASSERI

18.WANGASA

---------------------------------------------------------------------------------------------------------



WAKAMBA WALIUITA MLIMA HUU "KIMA JA JEU[MLIMA MWEUPE];WAMASAI WALIUITA"OL DONYO EIBOR"[MLIMA MWEUPE];WATAITA WALIUITA NJARO[KILIMA CHA MUNGU];WACHAGGA WALIUITA KIPOO[KIBO] AU KILIMA CHA NJARO [KILIMA CHA MUNGU]

------------------------------------------------------------------------------------------------------

"WELCOME TO TANZANIA THE LAND OF KILIMANJARO,ZANZIBAR,THE SERENGETI AND THE BUSINESS BRIDGE TO GREAT LAKES COUNTRIES VIA DAR ES SALAAM PORT"

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

Interestedtips said...

umenikumbusha nikiwa kwenye Train halafu nifike Dodoma.......safi sana

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa historia fupi ya kabila la kichaga...

Dada mdogo Ester..ni furaha kwangu kusikia umekumbuka hilo:-)