Tuesday, October 11, 2011

SAFARI YETU YA NYUMBANI TANZANIA HATUKUKOSA KUWASALIMIA MARAFIKI/WENYEJI WETU PIA:SHAMBA LA KAKAO HAPA NI MATEMA BEACH

Hapa ni mwenyeji wetu Mr. Mgaya ,akitutembeza katika moja ya shamba lake la kakao. Kwa sisi ilikuwa ni mara ya kwanza kuona ZAO hili la kako ni vipi linalimwa na linaonekana vipi. Maana tulikuwa tunaona kako ipo kwenye kopo tu tayari kwa kunywewa.

Na hapa ni mti wa kako na hizo unazoona zimeningínia ndizo kakao zenyewe hapo bado hazijaiva bado.
Ukimwa mdadisi basi utajifunza mengi ...Yaani nina maana tuliuliza kama kakao zinaliwa kkama zilivyo ..hapo ni matokeo yake tukatafutiwa maoja iliyoiva ikabanguliwa na tukaonja ..sikuwahi kuonja kakao freshi maishani ...ulikuwa msafara ambao tulijifunza mengi sana....

Hapa ni kako zimeanikwa na baadaye zitakuwa tayari kwa kuwa kakao ya unga ..tulishindwa kusubiri mpaka kunywa...Safari nyingine labda.... tembea uone mengi, uliza jifunze mengi nk nk, haya ndio maisha ... kuna mengi yanakuja!!!

4 comments:

ray njau said...

"MAMBO YA KILIMO KWANZA KWETU TZ."

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli maisha bila kila hayatakuwa maisha. Hata kama una kazi ya ofisi lazima kilimo kiwe mstari wa mbele.

ray njau said...

Na Yehova Mungu akamchukua mtu na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza._Mwanzo 2:15

Simon Kitururu said...

Zao hili Afrika Magharibi linadaiwa kushurutisha watoto kiutumwa sana tu lakini!

Na maajabu ya Musa ni kwamba nchi maarufu kwa kunywa kakao, kutengeneza chokoleti nk.... wala hazina mashamba haya ya kakao

Tembea ujionee, ... lakini ukishaona kama kifunzwacho hakigeuki tatuzi kivitendo,...
.. mtu usishangae USWISI au tu UBELIGIJI ,.... ndio wasifikao kwa kakao na machokoleti hata baada ya miaka mia kutoka sasa wakati Tanzania au Ivory Coast waongozao kwa zao hili bidhaa zao hazionekani sokoni.... kama tu katika kahawa ilivyo kuanzia katika makapuchino ,.. malate .. na vikorokocho vingine kuwa na majina ya KIITALIANO ambao kwenye kahawa hawana shamba.

Ni mtazamo tu!