Thursday, October 13, 2011

PICHA YA/ZA WIKI:-SARE SARE MAUA ASIYEJUA KUCHAGUA KABILA YAKE ....

Dada Rachel

Hapa ni mama/dada wa Swahili na waswahili yupo ndani ya T-shirt ya TANZANIA na ......


Dada Yasinta/Kapulya
...ni mama/dada wa Maisha na Mafanikio naye hayupo nyuma tena kavilia hadi kitambaa/bendera kichwani..wamependeza :-)

12 comments:

Simon Kitururu said...

Mmependeza WADADA!

Rachel Siwa said...

Asante MKAKA!

da,yasinta unavituko wewe kwikwikwi, ASIYEJUA KUCHAGUA KABILA YAKE SIJUI KWA NINI TULIKUWA TUNASEMA MZIGUA? Samahani Wazigua.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante MKAKA Simon!

Rachel! si unajua tena ukiwa Kapulya ...Haya bwana hata mimi sijui kwa nini tulikuwa tukisema mzigua/mzegua..labda kuna anayejua jamani tusaidieni!!!

isaackin said...

mumependeza wenyewe,tatizo ni hao viongozi wanaaoongoza hiyo nchi yenye hilo jina wanatuchanganya kwakweli

Mija Shija Sayi said...

Kaka Isaac usitie shaka wanawake wa shoka hao wameshakaa mstari wa mbele kuipigania nchi yao..Hizo Sare walizovaa zimeshikilia ujumbe mzito sana, kwamba kaeni chonjo TANZANIA wanawake tunakuja kuikamata NCHI...

Ngoja nami nikaitafute yangu tuanze kupiga kazi..

Goodman Manyanya Phiri said...

Rachel naye Yasinta kama ndugu vile hapa!!!??? Picha hizi ndio namna ya kutuambia sisi nyie ndugu... au...????

(miaka yangu hamsini inatosha, nyie Ndugu; na msinizeeshe zaidi!!!)

sam mbogo said...

Sisi enzi zetu tuliiba sale sale maua asiye juwa kuchagua kabila lake.. mgoni. tehe ...tehe... tehe...
mmetoka bomba mbaya,kudadadeki!! kaka s

MAMA LULU said...

mmependeza wadada,Tanzania OYEE,mnawakilisha vema.kuhusu kabila lake mzigua mimi nafikiri ni kutokana na ASIYEJUA kuchagua na MZIGUA,huwezi kusema asiyejua kuchagua kabila lake mngoniau mluguru.ni mambo ya MISEMO TUU.

mangi said...

Akina msitudanganye kabisa!Tuonyesheni kitu kipya na kamili kwa kuvaa mavazi ya wanawake katika picha kamili kuanzia juu kwenda chini mkionyesha uwakilishi wa kitanzania.

Simon Kitururu said...

Ghafla naamia upande wa mtani wangu MANGI ,...
... nahisi kuna kitu hamjatuonyesha. Na neno la MANGI liheshimiwe nanyi. Amen.

Swali la kizushi: Hivi ni SALE SALE au SARE SARE?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa kuwa nasi hapa
Ndugu Mamngi na kaka Simon nitawajibu...:-)

Rachel Siwa said...

nami nitawajibu dada Yasinta!.