Monday, October 10, 2011

MALI NA FEDHA NI KITU GANI KWA MWANAMKE?

Kuna jambo moja leo nataka kulizungumzia, nalo sio jingine bali ni hili la wanaume kutokujua hasa sisi wanawake tunawapendea nini katika ndoa au mahusiano.
Katika maisha yangu ya ndoa nimekuja kugundua mambo mengi sana ambayo huenda wanaume wengi hawayafahamu juu yetu sisi wanawake.

Kuna ujinga mkubwa sana ambao huwa unawasumbua wanaume. Wanaume wengi, sijui ni kutokana na malezi huwa wanadhani kwamba sisi wanawake tunahitaji fedha na mali ili kufurahia maisha ya ndoa au mahusiano.

Na dhana hii ambayo mimi naiona kama ni potofu, huwafanya wanaume kuamini kwamba wakiwa na fedha watakuwa wamemaliza matatizo yote ya mwanamke, na hivyo kuwa na ndoa au mahusiano yenye amani na utulivu.

Na kwa kuwa wanaamini hivyo, basi wakiishiwa ndani hapakaliki, wanahangaika kutafuta fedha ili kuzihami ndoa zao au mahusiano yao na wapenzi wao, kwani wanaamini kuwa bila fedha kutakuwa hakuna upendo tena kutoka kwa wake zao aua wapenzi wao.
Katika kipindi hicho cha ufukara ndipo mwanaume atakuwa karibu zaidi na mke au mpenzi wake kwa hofu ya kuogopa kuachwa, lakini baadae akizipata anakuwa hana muda na (bize)unajitokeza kwani wanakuwa na imani kuwa fedha ipo kwa hiyo uwezekano wa kuachwa na wake au wapenzi wao nao unakuwa haupo.

Sikatai wanaume kutafuta fedha kwa bidii ili kuondokana na umasikini na kuweza kijikimu kifamilia, lakini inapokuja kuonekana kuwa sisi wanawake tunawapenda wanaume kutokana na kuwa na fedha, hilo nalipinga kabisa.
Tuachane na zile dhana zilizojengeka siku hizi kuwa, wanawake wa siku hizi eti wanafuata pesa tu (after money) na wanathamini sana wanaume wenye fedha. Hilo inawezekana lipo lakini hebu tujiulize, hivi mwanamke anayempenda mwanaume kwa ajili ya fedha, hata akiolewa, unadhani atakuwa na amani kweli?

Kama mwanaume huyo atakuwa (bize) hana muda na shughuli zake, halafu anadai kuwa ana amani, basi labda atakuwa anaipata mahali pengine na sio kwa mume huyo, na hiyo ni hatari sana.
Kuna haja ya wanaume kujiangalia mienendo yao, je wanakuwa na muda na wake au wapenzi wao? Na wanatenga muda maalum wa kuzungumzia matatizo ya familia yao na kutafuta suluhu kwa pamoja?

Kuna haja ya wanaume kujikagua na kuangalia upya mahusiano na wake au wapenzi wao yakoje kabla mambo hayajaharibika

15 comments:

Mija Shija Sayi said...

Sema Yasinta sema. Wanaume walio wengi wanahitaji kubadili fikra zao juu ya maisha ya ndoa, na hili halitakaa liwezekane hadi watakapokubali kwa mioyo yao wenyewe kwamba maisha ya familia ni kukaa na kuzungumza pamoja juu ya kuiboresha familia na si kuziachia pesa zichukue nafasi hiyo...pesa si kila kitu..

Simon Kitururu said...

Je mwandishi anaongelea WANAWAKE wote katika dunia hii ambayo labda KUJENEROLAIZI yaweza kuwa ni hadaa?

Ndio nakubali kisemwacho na mwandishi ingawa nakumbusha tu ni hatari sana saa nyingine kuamini kuwa kwakuwa kwa mtu samaki ana shombo basi kwa watu wote samaki wananuka na sio kunukia.

Na baada ya hapo. Labda kuna MWANAMKE mali na FEDHA ndio kila kitu kutoka moyoni mwake kabisaa!

Ni mtazamo tu !

sam mbogo said...

Mali na fedha,ni msingi mkubwa kwa baadhi ya wana wake. pia jaribu kukumbuka wewe na huyo ama mkeo /mume wasasa hivi,kwa mara ya kwanza mlikutana wapi.mimi naamini wa kati mwingine kwamba wewe mwanaume ulikutana na huyo mkeo wapi mpaka mkaoana,vivyo hivyo kwa mwanamke.ukikumbuka hili yaweza kukupa picha kamali ya penzi lenu kama limetawaliwa napesa mali,nk. kwa maana hiyo kipengere cha mazingira yaliyo wakutanisha ninyi nimuhimusana katika kumuwajibisha mwanaume huyo mfikiria kuwa mwanamke ni fedha namali nitajaribu labda baadae kutoa mifano, ukweli swala hili lipo. kaka s

Baraka Chibiriti said...

Ila Dada Yasinta ukubali usikubali, wanawake wa kibongo wanajali sana mshiko, yaani hilo lipo kabisa tena wazi wazi tu. Wewe unatambua hivi kwasababu umejifunza mengi sana hasa kwa kukaa nje ya nchi. Yaani hili kwa Tanzania yetu nimelichunguza sana wasichana wengi sana wanapenda hela tu. Mimi kabla sijaja huku Ugaibuni kuna msichana nilitokea kumpenda sana tena sana, nilifanya kila mbinu ili niwe naye, lakini alinitolea nje tena mbali tu na kutoa sababu kibao. Aliposikia tu nimekuja huku, mara barua za mapenzi zikaanza kumiminika kwangu, kuwa nakupenda sana napenda tufunge ndoa. Nami nilimsoma tu, nikakubali nikimtega. Mara maombi yakaanza kumiminika, nikamwambia sina kitu kabisa, na kumwambia; tena wewe unaweza ukawa umenizidi sana tu kiuchumi usitishike kuwa Ulaya. Mara nikaona kimya, akasepa kabisa. Haya ni mengi tu kwa kwetu, ningeweza kukuhadisia mengi tu ila hilo naamini linatosha. Kweli kabisa kwa wanawake wa kwetu walio wengi sana wanaangalia mali tu!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Da Yasinta umesahau kale kamsemo-HAPENDWI MTU HAPA POCHI LAKO TU?

kiuhalisia utakuta baadhi ya wa dada wa siku hiziwana VIDUMU..mmoja ATM, mwingine wa kitandani na mwingine mwenye mvuto wa kutoka naye!!!

Nakubaliana kimtindo na Mt Simon, Kaka Sam na Kaka Kibiriti

Yasinta Ngonyani said...

Haya ndugu zanguni...mimi nataka kutofautiana tena kidogo nanyi ...KUPENDA...MALI/PESA..ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama kweli mtu anampenda mtu basi atampenda na atamkubali kama alivyo hilo ndio penzi la dhati. KWASABABU MTU UNAPOOLEWA OU UNACHOTAKA NI MKE/MUME ambaye unaweza kuwa nanye . na sio hela. Sikatai kwamba hele/mali ni muhimu hapana. LAKINI KIKUBWA ZAIDI HAPA NI LILE PENDO LA DHATI AKIWA KILEMA, MASKINI....nanyi ni ruksa kuwa tofauti nami hii ndio sababu ya mjadala.

sam mbogo said...

Yasinta,sasa hivi siyo siri,watu wakariba yako wanaothamini kwanza penzi na pesa mali nimatokeo niwachache sana tena wa kutafuta kwelikweli. na kwa taarifa yako ukikaa mkao fulani au kona fulani unaweza kumshitukia kuwa mwana mke ndiyo anayesababisha wanaume tuseme/waseme wanawake wana jalipesa namali kuliko penzi,je mfano wa bwana Chibiriti unaufikiriaje? kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo kaka S. Nakuelewa sana na wengine wote nimewaelewa sana..Labda naweza kuongezea ya kwamba pesa ndio mwanamke na mwanamke ndio pesa..Na huo mfano wa kaka Chibiriti naamini upo na unaendelea kuwepo na hiyo ni wazi kabisa hapa hakuna PENZI...labda ni kweli watu tupo tofauti kwa kuthamini kitu na mtu.

ray njau said...

KIELELEZO KWA WAUME

5 Biblia inasema kwamba waume wanapaswa kuwatendea wake zao jinsi Yesu alivyowatendea wanafunzi wake. Fikiria mwongozo huu wa Biblia: “Waume, endeleeni kuwapenda wake zenu, kama vile Kristo pia alivyolipenda kutaniko na kujitoa mwenyewe kwa ajili yake . . . Vivyo hivyo, waume wanapaswa kuwa wakiwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Yeye anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe, kwa maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake kwa vyovyote; bali huulisha na kuutunza kwa upendo, kama vile Kristo pia anavyolitendea kutaniko.”—Waefeso 5:23, 25-29.

6 Upendo wa Yesu kwa wanafunzi wake ni kielelezo bora kwa waume. Yesu ‘aliwapenda mpaka mwisho,’ akadhabihu uhai wake kwa ajili yao, hata ingawa hawakuwa wakamilifu. (Yohana 13:1; 15:13) Vivyo hivyo, waume wanahimizwa hivi: “Endeleeni kuwapenda wake zenu nanyi msiwakasirikie kwa uchungu.” (Wakolosai 3:19) Ni nini kitakachomsaidia mume kufuata shauri hilo, hasa ikiwa nyakati nyingine mke wake hatendi kwa busara? Anapaswa kukumbuka makosa yake na anachopaswa kufanya ili kupata msamaha wa Mungu. Anapaswa kufanya nini? Anapaswa kumsamehe kila mtu anayemkosea, kutia ndani mke wake. Bila shaka, mke anapaswa kufanya vivyo hivyo. (Mathayo 6:12, 14, 15) Je, unaona ni kwa nini watu fulani husema kwamba ili ndoa zifanikiwe lazima wenzi wote wawili wawe tayari kusameheana?

7 Waume wanapaswa kukumbuka pia kwamba sikuzote Yesu aliwajali wanafunzi wake. Alizingatia udhaifu wao na mahitaji yao ya kimwili. Kwa mfano, alisema hivi walipokuwa wamechoka: “Njooni, ninyi wenyewe, faraghani katika mahali pasipo na watu mpumzike kidogo.” (Marko 6:30-32) Wake pia wanastahili kuhangaikiwa kwa upendo. Biblia husema kwamba wao ni “chombo dhaifu zaidi” na waume wanaamriwa wawape “heshima.” Kwa nini? Kwa kuwa waume na wake pia wanashiriki “pendeleo lisilostahiliwa la uzima.” (1 Petro 3:7) Waume wanapaswa kukumbuka kwamba Mungu hupendezwa na uaminifu wa mtu wala si jinsia yake.—Zaburi 101:6.

8 Biblia inasema kwamba mume “anayempenda mke wake anajipenda mwenyewe.” Hiyo ni kwa sababu mume na mke “si wawili tena, bali mwili mmoja,” kama Yesu alivyosema. (Mathayo 19:6) Hivyo basi, hawapaswi kufanya ngono na mtu mwingine yeyote. (Methali 5:15-21; Waebrania 13:4) Wataepuka kufanya hivyo ikiwa kila mmoja anajali mahitaji ya yule mwingine bila ubinafsi. (1 Wakorintho 7:3-5) Kikumbusho hiki pia kinafaa: “Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake kwa vyovyote; bali huulisha na kuutunza kwa upendo.” Waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama wanavyojipenda wenyewe, wakikumbuka kwamba watatoa hesabu kwa Yesu Kristo, aliye kichwa chao.—Waefeso 5:29; 1 Wakorintho 11:3.

9 Mtume Paulo alizungumzia ‘upendo mwororo alio nao Kristo Yesu.’ (Wafilipi 1:8) Wororo wa Yesu ulikuwa sifa yenye kuburudisha, iliyowavutia wanawake ambao walikuwa wanafunzi wake. (Yohana 20:1, 11-13, 16) Nao wake hutamani sana waume zao wawapende kwa wororo.

sambogo said...

Amina. mungu nimkubwa kaka S.

MARKUS MPANGALA said...

Labda kwakuwa sijaoa, lakini nimesoma maelezo yatokanayo na Biblia kuna wakati yanaibuka maswali ambayo sidhani kama yatapatiwa majibu maridhawa.

Pengine siyo muhimu kupata majibu, lakini kuna tatizo, hata kama halisemwi sana au baadhi kutokuwepo kwenye kundi la wapenda mali. na sisemi kuwa wapenda mali ni wabaya, lakini kuna kulemazwa sana kifikra. Nadhani hili kaka Shaban Kaluse analijua katika utambuzi. Yapo mengi mitaani, yanakera.

MATHALANI MFANYAKAZI:
analipwa 100,000/= kwa mwezi lakini mshahara wake unakaa siku 4 tu halafu orodha ya mahitaji inahamia kwa mwanaume; sina nauli,nataka kwenda saluni, ninamboa sina hela ya matuzi, nataka kununua hiki ama kile. labda hili ni dogo tu, lakini vipi wanaoolewa? mifano ni mingi ila inachosha kutaja. kwa kuzungumzia kwetu hapa si rahisi kuwapata 100% ya wanawake wasipenda mali, na wengine wanajificha kwenye kichaka cha kusema "au unadhani nataka mali zako". hii ni kauli ya kawaida tu. lakini kuna mengi ya kufikiri kama siyo kutafakari. ni kweli wapo wanaume wanaodhani kuwa mali/pesa ni tiba, lakini swlai wanawake wangapi wanafikiria hizo pesa/mali? sizungumzii uzoefu maana wakati mwingine hautoi jawabu. si rahisi, kuna matatizo makubwa sana ya kisaikolojia. watu wanatisha kwa kweli,inaudhi. huwa najiuliza kwanini wanawake wanadhani mwanaume alipewa dunia kuitawala? fikra hizi zipo nyingi ndiyo maana utasikia ukombozi dhidi ya mwanamke, halafu wanasemna mfumo dume..... sijawahi kupata maelezo ya kutosha juu ya hoja hii ya mfumo dume. wanawake wamelemazwa sana, wapo wenye malezi ya hovyo,matendo ya hovyo na kudhani kuwa ukiwa na mpenzi/mume ni kutatua matatizo yote na wengine kabla ya kuingia kwenye uchumba/ndoa unaona orodha ya kero, unabaki kushangaa, inakuwaje? ni nani aatakayewadhuru wanawake ikiwa wana juhudi za kutenda mema? kwa hali ilivyo maisha ya mijini nyakati hizi, si rahisi kukubaliana na dadangu Yasinta. labda niseme pia ile hali inayomzunguka mtu, kune mengi ya kujadili hili, dada Yasinta uko kwenye ndoa, lakini wapo wanawake wana mengi ya ajabu. na kuna dhana moja kuwa 'wanawake ni ombaomba". samahani nawazungumzia hawa wanaojaribu kutaufuta kuishi maisha ya ndoa na kadhalika. nimeshuhudia baadhi ya wanaume wakiwabwaga wapenzi/wachumba zao, kisa MISS I WANT, MISS I NEED, MISS BUY ME SOMETHING, MISS I DON'T HAVE na meingineyo. Imenichukua muda kuja kuamini maana ya GOLDIGGERS. nadhani KANYE WEST alikuwa sahihi. kuna matatizo mengi sana hapa, kuna ndoa nilishuhudia mzozo kwakuwa mume alikuwa akikagua hesabu za ujenzi, badala ya mke kueleza anakimbilia kusema "kwani mi nataka mali zako". Kwa mtindo unaoendelea ni rahisi kusikia vijana wengi wanaahirisha kuoa/ nazungumzia upande wa wanaume

Anonymous said...

HALLO SIS, WEWE KWA SABABU UMESHATOKAMO. MIMI NI MWANAUME WA MIAK 45 SASA NIMEKUJA ULAYA TANGU NINA MIAKA 20. MAPENZI YANGU NIMEANZA NA MWANAMKE WA KIZUNGU MPAKA KUFIKIA UMRI WA MIAKA 41,MAISHA YALIKUWA POA WALA MWENZANGU HAJUI PESA WALA NINI TULICHOKUWA NACHO NDIO HIVYO TULIVYO BAJETI. IKATOKEA IBIRISI ETI NIMTAFUTE MWANAMKE WA BONGO NDIO NIMALIZIE MAISHA NAE NAJUTA WALA SINTOSAHAU! NI MWANAMKE TU WA FAMILIA YA KAWAIDA TENA USWAHA MBAGALA. HUYO SIS ANAPENDA PESA KAMA SIJUI NI NINI KILA SIKU NIMEFIWA NILNUNULIE KIATU KAMA KILE ALICHO VAA BEYONCE, KAMA LILE JEANS LA J LO, NA MAMBO MENGI TU.

MPAKA SIKU MOJA NIKAMWAMBIA SINA PESA YA KUKUNUNULIA VITU HIVYO MIMI NI MFANYAKAZI WA KAWAIDA TU. UNAJUA ALINAMBIA NINI? ETI NISAHAU SIWEZI KUMPATA MPENZI TANZANIA KAMA SINA KIPOCHI AU SIWEZI KUTOBOKA NA HUYO NDIO ALIKUWA WIFE MTARAJIWA!SASA MIMI SINA MAPENZI TENA NA DADA ZETU WA KIBONGO: NIMEAMUA KUFA NA ZERUZERU WETU HUKU HUKU. NINACHOTAKA KUSEMA NI KWAMBA HAKUNA PENZI TANZANIA KAMA HUNA POCHI LA KUTOSHA, WAO WANAJALI PESA KWANZA HATA FAMILIA YAKE WANAMUULIZA HUYO BWANA ANA PESA? KABLA YA YOTE KWA SABABU LAZIMA UKUNGUTISHWE NA FAMILIA YAKE YOTE

Anonymous said...

Haya makubwa hayo ndio ubongo huo wanafunzi wa kibongo ndiyo kama hivyo mnavyo ona kwenye vyombo vya habari huko KUALA LUMPA Malaysia wamecharuka kujiuza mpaka kijulikane wako mbioni kutafuta pesa na wao watakula polisi au penzi la mwanaume ?Asubuhi wanaamka njaa na wamekwisha fanywa usiju jucha wanasema mshiko kwanza

Goodman Manyanya Phiri said...

Mwanamke anaekusudia kuolewa na maskini ni mjinga na mpumbavu.

ray njau said...

WAHESHIMIWA MABIBI NA MABWANA TAFADHALI TEGENI MASIKIO YENU NA MFUNGUE MACHO YENU:
"NDOA BILA UPENDO NI DOA"