Thursday, October 13, 2011

HIKI NI KIFUNGUA KINYWA CHANGU CHA ASUBUHI YA LEO NI UJI WA ULEZI KARIBUNI!!

Karibuni tujumuike jamani ni uji wa ulezi...na wala msiwe na wasiwasi kuwa labda hautoshi kuna zaidi!!!



8 comments:

Anonymous said...

Aisee umenitamanisha sana uji waako maana mimi ni mlevi wa uji

Simon Kitururu said...

Mimi huo ulishanishinda. Uji kwa ujumla sijui kwanini huwa nauonisha na kuugua kutokea utotoni.

Mama yangu anadhani kunauwezekano kisaikolojia niliathirika kwa kuona wagonjwa wakibwia sana kitu hiyo kitu ambacho kimentoa hamu zake. :-(

Nilipokuwa shule ya bweni ambako UJI ilikuwa kifungua kinywa nifanikiwa kukondisheni mwili na kuruka kabisa swala la kifungua kinywa kama nimechacha na kushindwa kufungua kinywa kwa kidude kingine.


Kwa hiyo kiaina THANKS but NO thanks!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina nafurahi kukutamanisha ...umenifurahisha kwa kusema kuwa ni "mlevi wa uji"

Simon pole...ila usiache kuja kwa hilo utapata chai na chapati.

Rachel Siwa said...

Ahsante da'Yasinta naonaunameremeta sijui umeweka Siagi, mimi huupenda sana, je wewe unaupikaje?@ kaka wa mimi Kitururu Uji wa mchele jee unapanda? da'Yasinta mpe Chingambo huyo sina hakika na jina hilo.

Yasinta Ngonyani said...

Rachel wala sijaweka siagi na wala sijaweka sukari wala asali ni kama ulivyo...Jinsi ya kupika nimekologa na maji na kuchemsha mpaka kuchemka na nimechemsha zaidi dakika kama kumi hivi....Rachel una vituko wewe eti mpe chingambo...jina umepatia haswaa. Ngoja aje tuone kama huo uji wa mchele au hicho chingambo kinapanda...

Anonymous said...

umenikumbusha uji wa mbege dada yasinta yaani mama yngu alikuwa anaupenda ilikuwa spesho sana kwa mama ambaye ametoka kujifungua basi ukipikiwa wanatia maziwa mtindi na siagi na sukari yaani usiombe ni tamu je lakini nasikia kwa watu wenye matatizo ya moyo haiwafai kwa sabaubu inanguvu sana ni hayo tu umenitamanisha na mimi zisubutu kutumia na hii afya niliyonayo nitabaki kuangalia tu kwa macho

Goodman Manyanya Phiri said...

Uji huo ni rangi ya udongo pia ni rangi yako, chakula cha kwanza kwake Adam na Hawa!

ray njau said...

Akina msitudanganye kabisa!Tuonyesheni kitu kipya na kamili kwa kuvaa mavazi ya wanawake katika picha kamili kuanzia juu kwenda chini mkionyesha uwakilishi wa kitanzania.