Monday, October 24, 2011

CHUMBANI/CHUMBA CHA KULALA KIWEJE?

Habari zenu ndugu zangu natumaini wikiendi yenu wote imekuwa sio ya pilikapilika sana.

Haya mwenzenu leo nina swali ambalo limekuwa likinikera muda sasa. Lakini jana nilishindwa kuvumilia na wakati nipo kazini nikawauliza wafanyakazi wenzangu. Jambo lenyewe ni kuhusu chumba cha kulala. Na swali lenyewe ni hivi je? chumba cha kulala kinatawa kiweje? Yaani pembeni mwa chumba kuwa na vimeza na je hapa kwenye vimeza kuwe na nini? na je? kuwa na TV? Computer? na aina nyingine ya vitu? au kuwa na kitanda tu?...na baadaye baada ya pitapita /udadisi wangu nikakutana na habari hii hapa chini ambayo nimeiunganisha. haya tusaidiana kupeana ushauri.
---------------------------------------------------------------------------------------------

naamini baadaya ya siku ndefu kutafuta riziki, na baada ya siku ndefu kuongea na watu tofauti, kukasirishwa na watu tofauti na wakati mwengine inafika mda mwili wako unakuwa umechoka unachohitaji na kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani.. wengi nimesikia wakisema huwawia vigumu kupumzika vizuri kitanda kingine tofauti na alichonacho nyumbani.. sababu ni kwamba labda godoro la nyumbani ni zuri kuliko sehemu nyengine ama tu ukilala nyumbani unapumzika vizuri zaidi ukiwa pembeni ya mtu aliyekaribu na moyo wako..

ndio swala la chumbani linapoingia, sehemu ya kulala hupaswa kukufanya uchovu uliokuwa nao wote kutoweka, chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi vya kufanya hata hewa isiingie, sijui viatu, kapu la nguo chafu, ma vengine vingi.

hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda eote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa.

chumbani mambo mengi sana hufanyika ukiacha kulala, hata kupumzika tu na mwenzi wako mkiongelea mambo fulani ya maisha yenu. kwahiyo hutaki kufanya hivyo na harufu mbaya ikiwapitia pembeni. Habari hii nimekutana nayo hapa.

6 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

chumba cha kulala? wapi? uswazi ama mjini?

mambo ya tv ni ya mjini uswazi hakuna cha tv...

ray njau said...

"Hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda eote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa."
==================================
Zama hizo kulikuwa na somo la 'maarifa ya nyumbani' na siku hizi sijui wanasema 'stadi za kazi'.
===================================
Ni ukweli mtupu kuwa iwe uswazi iwe site senta dhana ni moja tu kwa wadau wote kuwa chumbani ni sehemu sana katika maisha ya binadamu na kudumisha hali ya shaghalabagala au hobelahobela ni hatari sana kwa siha njema na pumziko maridhawa.

Fadhy Mtanga said...

Sijapita humu kibarazani siku nyingi sana kutokana na mambo chungumbovu.

chumba cha kulala, ni sehemu ninayoihusudu zaidi nyumbani ingawa huwa nalala masaa machache sana!

Simon Kitururu said...

Mambo ya TV na kuingia kwenye Facebook au tu kufanyakazi kwenye Kompyuta Chumbani ni moja ya kiuacho mawasiliano kama unamtu .

Kwa ujumla less is more chumbani.Kisichohusiana na kulala au angalau chakula cha usiku na kisiwe chumbani ikiwezekana.

Sophie B. said...

Yasinta sasa naona unanambia niweke bidii zaidi maana kwenye blog zangu kama somo hili halijaeleweka.
Haya kwetu wapambaji tunasema Chumba cha kulala kiwe
kitanda na vimeza vidogo 2 (night tables) kila upande.
Hapo unaweka taa au glasi ya maji au kitabu/biblia.
pia kuwe na kiti kimoja ambapo mtu anaweza kukaa.
kuwena angalia picha moja au 2 ukutani kupendezesha mfano picha hizi za kuchora.
kama hakuna kabati la ukutani basi kabati liwepo moja na kama kaka ray njau alivyosema likae limefungwa.Kusiwe na tv au kompyuta.
picha hapahttp://sophiasclub.blogspot.com/search/label/Upambaji%20chumba%20cha%20kulala na hapahttp://absolutelyawesomethings.blogspot.com/search/label/bedrooms

Unknown said...

Safi nimeelewa nilikuwa sijui kuhusiana na maandaliz ya Room ila now nimeelewa..ila thanks🙏🙏🙏🙏