Friday, October 28, 2011

NIMEIPENDA HII PICHA NA NIMEONA IWE PICHA YA WIKI!!

kuoa katika umri wa miaka 120.

Kwa maelezo zaidi ingia HAPA

13 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

Safiii sana ila sijajuwa kama kweli ameoa kwa nia ya kuoa ila inawezekana kaenda kufuata ujane na kurithi mali sitaunga mkono wa kumpatia hongera kwa kuoa ila pole kwa kuoa au kuolewa
Che Jiah

Anonymous said...

MALOVE[MAPENZI]HANA UMRI,JINSIA WALA KABILA NA KAMWE USIJIINGIZE KATIKATI YA MALOVE YA WAWILI WALIOAMUA KWA MOYO DHATI KUUNGANA KATIKA MAISHA YA FAMILIA.
------------------------------------
"HONGERENI SANA BIBI NA BABU ARUSI"
-----------------------------------


R.Njau

Simon Kitururu said...

Anacheti cha kuzaliwa huyo?
Mengine jamaa wamenisemea!

Ingawa nahisi MALOVE fulani yana UMRI maana binti yangu mwenye miaka mitano nikimkuta anatongozwa na libaba zee hata kama linampenda kikweli hilo LIBABAB chamoto litakiona!:-(

Na ndio ,..
.. kuna waoao kutafuta trekta kiukulima shamba, mpishi au tu mfuaji kisa kama huyo ni mke kisheria hana mshahara katika mila nyingi.:-(

Unknown said...

Mmmh...ngoja Nami nikitururize....

ray njau said...

Ndoa ni maridhiano ya wawili ambao kwa ridhaa wamekubaliana kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kimungu na serikali na vigezo na masharti kuzingatiwa.

Simon Kitururu said...

@MANGI a.k.a Mtani wangu Mkuu NJAU: Tatizo watu husahau NDOA na MAPENZI ni vitu viwili tofauti na ndio maana kwa kuridhiana kuna mpaka vipengele NAJISI hununulika kwa kuwa KURIDHIANA si lazima ni PENZI.

Na kwa bahati mbaya MUNGU hutegemea unaamini MUNGU ni nini au tu ni NANI!:-(

AU?

Ni mtazamo WANGU tu huu!

ray njau said...

Mtani wangu naomba nikuulize swali hili:"Ndoa bila mapenzi itakuwa ndoa au ndoana"?

Simon Kitururu said...

@Mtani Njau: Ndo siku hizi si nasikia ni neno tu?

Na nasikia NDOA YOYOTE ile ni NDOANA kwa kuwa lazima kinamna MTU kadakwa.

ray njau said...

@Mtani:S.Kitururu;
Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.Ndoa ni mradi kama miradi mingine maishani na kamwe usiwe muoga na kuunyima moyo wako kile ambacho ni haki yake kukukipata katika uwezo wa maamuzi na mikono yako.Usifikirie namna ya kuvuka daraja ambalo hujalifikia na kamwe usijenge hisia za ndoa kuwa doa au ndoana wakati hata sura ya laazizi nyongo mkaa na ini haijulikani.Ndoa ni sehemu muhimu sana katika maisha ya binadamu lakini kuoa siyo jambo la kuumiza kichwa bali namna ya kudumisha maisha na mafanikio ndani ya mikikimikiki ya ndoa.["A house is made of bricks and stone but home(marriage) is made of 'LOVE' alone].
Na Yehova Mungu akaendelea kusema: “Si vema huyo mwanamume aendelee kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi, awe kikamilisho chake."Kwa hiyo Yehova Mungu akamletea huyo mwanamume usingizi mzito, na alipokuwa akilala, akachukua ubavu wake mmoja na kisha akafunika nyama mahali pake. Na Yehova Mungu akaufanya ubavu ambao alikuwa ameuchukua kutoka kwa mwanamume kuwa mwanamke na kumleta kwa huyo mwanamume. Ndipo huyo mwanamume akasema:
“Mwishowe huyu ni mfupa wa mifupa yangu
Na nyama ya nyama yangu.
Huyu ataitwa Mwanamke,
Kwa sababu huyu alitolewa katika mwanamume.”
Hiyo ndiyo sababu mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake nao watakuwa mwili mmoja.Na wote wawili walikuwa uchi, huyo mwanamume na mke wake, lakini hawakuona haya.-Mwanzo 2:18,21-25.

ray njau said...

Mtendaji mkuu na wadau wote wa maisha na mafanikio nawatakieni wikiendi njema yenye mafanikio kimaisha na msisahau mikikimikiki ni sehemu ya maisha na mafanikio.Wakati wowote na popote ulipo tembelea na uwe mfuasi wa blogu ya maisha ni mikikimikiki.
===================================
"FURAHA NA AMANI VITAWALE KATIKA NDOA NA FAMILIA ZA WADAU WOTE NA WASOMAJI WA BLOGU ZA MAISHA NA MAFANIKIO NA MAISHA NI MIKIKIMIKIKI."
===================================

Simon Kitururu said...

@Mtani Ray NJAU

Asante Mkuu Njau kwa mahubiri na kwako pale MAISHA ni MIKIKIMIKIKI mie tayari mwenyeji.

Swali la kizushi:
Hivi wewe MCHUNGAJI nini maana huchezi mbali na nukuu za BIBLIA?...


...kitu ambacho ni bomba la kitu kwa waaminio BIBLIA ni neno SAHIHI ... kitu ambacho MABUDDHA au WAISLAMU sijui kimanati wanalengwaje ili WATHIBITISHIWE kiimani kama waaminio BIBLIA waaminivyo BIBLIA ni KWELI TUPU na hakuna mkono wa MTU!


Ni kamtazamo kangu kwa SAUTI!
WIKIENDI NJEMA KWAKO PIA NGULI!

Salehe Msanda said...

Du: inapendeza

Kila la kheri

ray njau said...

@Mtani wangu S.Kituru;
Asante sana kwa pongezi zako na salamu maridhawa za wikiendi.Mimi siyo mchungaji bali msomaji biblia nikiwa mmoja wa mashahidi wa Yehova.Programu za mashahidi wa Yehova zinatayarishwa katika msingi wa kumfanya mtu awe mwanafunzi na mwalimu wa neno la Mungu.Waislamu na Wabuddha wanameteyarihiwa programu zao zinazowawezeha kunufaika na biblia.Kwa habari zaidi tafadhali tembelea www.watchtower.org.