Wednesday, June 6, 2012

SALAMU NI NUSU YA KUONANA

Au tu kwa vile ni jumatano ya marudio basi ngoje turudie  na hii. nimeipata hapa
Tusalimiane japo kwa maneno machache wakati wowote bila kujali majukumu yetu ndani mikikimikiki ya maisha kwa kuwa kila mmoja anamhitaji mwenzake kwa nyakati tofauti ijapokuwa nyakati nyingine waweza kuhisi kuwa mtu fulani siyo muhimu sana kwako lakini wakati wa uhitaji ndiyo unatambua bila fulani mchakato wa maisha na mafanikio hauwezi kufikia tamati.
Kama wingi wa viungo mwilini kwa kutazama lakini wakati wa mahitaji kila kimoja kwa nafasi yake humtimizia binadamu haja yake.
"Salamu ni daraja la urafiki"
Wasalamu na shukrani;
 

JUMATANO NJEMA!!!

4 comments:

ray njau said...

Hakika salamu ni ufunguo maisha na mafanikio kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.Je wewe umewasalimia watu wangapi leo?

Yasinta Ngonyani said...

labda Ishirini au zaidi!!

Mija Shija Sayi said...

Ujumbe huu umenikumbusha salamu za redio Tz, nani anakumbuka majina ya wanasalamu mashuhuri? ghafla majina yamenitoka...

Ubarikiwe Yasinta na wote watakaopitia hapa..

serinaserina said...

Kila kimoja kwa nafasi yake... mawaidha mazuri sana Da Yasinta