Saturday, June 9, 2012

JUMAMOSI YA LEO MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUANGALIA KIPAJI CHA DADA HUYU!!! HUKO MJI KASORO MAJI/BAHARI MAROGORO!


Nawatakieni JUMAMOSI NJEMA WOTE.....

7 comments:

nyahbingi worrior. said...

siku njema.Hivi bila kuwezeshwa kipaji kinaweza kuonekana?Kwa mfano Diego alikuwa na kipaji,kikakuzwa na waliomwezesha,Tyson Mike alikuwa na kipaji lakini kilikuzwa na wawezeshaji.

Je sisi tuna wawezeshaji wa vipaji?

nyahbingi worrior. said...

...sio wawekezaji....

Amani.

Yasinta Ngonyani said...

kaka nyahbingi worrior..hapa ndipo nilipotaka kufika ni kwamba kuna watoto/watu wengi wana vipaji vya ajabu lakini wanaachwa tu na mwishi vinakufa hivihvi ni jambo la kusikitisha kwa kweli.

Rachel siwa Isaac said...

Hongera zake dada huyu,kila siku namuangalia weee, lakini ataishia kucheza sokoni tuu kumi kumi tunacheka,mwehh Mungu amsaidie apate wawezeshaji!!

ray njau said...

Yasinta;
Jina la kibaraza ni maisha na mafanikio.Hapa tusianze kunyoosheana vidole bali kupitia kibaraza hiki tumtafutie muongozo wa kuwaona wahusika na wao kwa nafasi yao wanaweza kumvusha daraja na kuifikia 'nchi ya maisha na mafanikio'.Kupitia baraza la sanaa la Taifa anaweza kuelekezwa wadau anaoweza kuwaona kwa ajili ya kupima uwezo wake katika tasnia ya muziki na kupromoti kazi zake kwa umma.

ray njau said...

Daima penye nia pana njia na penye maisha pana mafanikio.Nawatakia wadau wote wikiendi njema sana kifamilia.
-------------------------------------
Asanteni na kwaherini kwa sasa!!

Festo Tarimo said...

Asante Dada Yasinta umenipa changamoto kupitia kwa Huyu Dada Wa Morogoro, sasa Yale nilokuwa nahofia siyawezi nitayafanya kwa Ujasiri mkubwa na Hakika nitashinda.