Thursday, June 14, 2012

TUSISAHAU SANAA NA UTAMADUNI..NIMEPENDA SANA VINYAGO HIVI/HIKI!!!


Hii picha/kinyago nakipenda sana ..ila huwa najuuliza kwanini nakipenda? Na pia najiuliza kwa nini mtu aliyetengeneza hakutengeneza na mikono ? Na pia mguu mmoja tu?  Mmmmmhhh !!! Je wewe mwenzangu unafikiri alifikiri nini  mchongaji?

Au kama hivi hapa yaani mikono jamani imepata kipaji ambacho hakiwezi kusimulika. Hapa ni mke ma mume wakiwa wameshika jembe na shoka lakini bahati mbaya shoka la mama lienipotea na umebaki mpini tu. Hii nilipata zawadi kwa rafiki yangu Joyce toka Njombe. AHSANTE JOYCE!!!!!

4 comments:

Ester Ulaya said...

WACHONGA VINYAGO WANA MAANA SANA KWA KILA KINYAGO, MIMI HUWA SIWEZI KUVITAFSIRI, ILA ALIYEKICHONGA UKIMUULIZA ATAKUPA MAANA YAKE, BIG UP WACHONGAJI

serina said...

Zawadi ya kufaa kweli...

Yasinta Ngonyani said...

Ester! umenena kweli, labda nilifanya vibaya sikuuliza niliponunua... Hakika watu wana vipaji na hasa ukifikiria ni mikono ya watu hiyo HAKIKA NAWAPONGEZA SANA pia namshukuru Mungu kwa kunipa mikono mie pia.
Serina! yaani hii ni kufaa kwelikweli:-)

Rachel siwa Isaac said...

Kila mtu anamikono da'Kadala lakini kila mmoja anaitumia tofauti na mwinngine,Mungu anaweza yote, ya'Kadala si ya Kadoda na ya kadoda si ya Kachiki!!!!!!