Tuesday, June 19, 2012

UJUMBE WA JUMANNE HII !!!NI KAMA IFUATAVYO....!!!!

Katika dunia hii sio wote ambao wanakupenda. Lakini kama unajipenda mwenyewe huna sababu ya kuwa na wasiwasi. Kuwa na furaha.Na kumbuka Mungu anakupenda. KILA LA KHERI WA WOTE!!!

6 comments:

Ester Ulaya said...

Shukrani sana kwa ujumbe mtamu wa leo

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha kwangu kufikisha ujumbe na nafurahi kama umekuwa mtamu kwako Ester. Ahsante sana.

nyahbingi worrior. said...

Basi kama kuna mtu anaweza kusahau kama Mungu anampenda,itakuwa tatizo.

Sellai I.

sam mbogo said...

Kwa ufahamu wangu,binaadamu kujipenda mwenyewe kwa dhati ,nina hakika hakuna.kama tungejipenda wenyewe kwa dhati basi leohii dunia hii ingekuwa swali. mfano mdogo tu ikiwa utajipenda wewe mwenyewe kwa dhati,huta kaa kufikiri ya mwengine akuharibie siku.ila ninacho juwa mimi kila kitu ni kwa kiasi. kaka s

ray njau said...

Zilongwa mbali,zitendwa mbali[zilongwazo siyo zitendwazo].Wanaimba kijamaa wanacheza kibepari.Upendo ndiyo msingi na daraja la maisha na mafanikio.Je ni kweli mimi na wewe tunafanya yote tuwezayo kwa kuonyeshana upendo kupitia matendo yetu na siyo midomo yetu?

Yasinta Ngonyani said...

nyahbingi worrior! Amini nakwambia kuna wanaoamini hakuna Mungu na kama hawaamini kuna Mungu je watajuaje kama anawapenda?

Kaka Sam! hapa nilikuwa namaanisha huwezi kumpenda mtu mwingine kama hujipendi mwenyewe.. inakuwa rahisi ukijipenda mwenyewe kwanza yaani kujiona nawe ni binadamu katika ulimwengu huu...

Kaka Ray..kwanza ahsante kwa wimbo ..pili inawezekana tunatenda na hatujui.