Monday, June 11, 2012

KAPULYA NA BUSTANI YAKE LEO....

Kama wengi mnakumbuka wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na shughuli ya kulima bustani  kwa hiyo  hapa ni mwendolezo au niseme .....


 inaendelea kama muonavyo hapa ni leo na mimea imeanza kuchipua ukiangalia sana utaona
....mdada anaendelea kumwangilia ili mimea ikua kwa haraka  mpiga picha ni dada Camilla...haya tutaendelea kuona mafanikia baada ya wiki tena...JUMATATU NJEMA NA JIONI NJEMA ....

14 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kazana Kapulya. Hata mimi nataka kuanza tena kwani msimu wa bamia, matango na matikiti maji ndo hasa umefika....

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Matondo! yaani umeniumiza roho kweli kujua huko unaweza kulima bamia, matango na matikiti maji..unaliama hivi nje mkama mimi au unalima kwenye nyumba (greenhouse)?

Mija Shija Sayi said...

Kweli kila mtu na karama yake..

Hii bustani umeipangilia si mchezo, mimi nisingewaza hivyo... sasa hayo magunia ndo umefunika mbegu au?

Yasinta Ngonyani said...

Mija hakuna kitu kizuri kama kucheza na udongo..yaani raha kweli halafu fikiria baada ya wiki ni kutoka tu nje na kuchuma mchicha wangu...Si magunia na wewe vaa hiyo miwani vizuri ni mifuko nazuia ili nyasi zisite kwa haraka...

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana da'Kadala!!!

sam mbogo said...

mwanamke vikuku mguuni wacha weeee!! Yasinta unatisha hapo uko kwenye kibustani! safi mkulima mzuri wa ulaya.haya mavuno mema. kaka s

nyahbingi worrior. said...

Kweli ulaya ni ulaya.Bustani ya huku na Ulaya zinatofautina kwa asilimia kubwa.

Penina Simon said...

Bigup, nimependa bustani yako, mboga zikikua ntakuja kula.

Ester Ulaya said...

ngoja niandae unga wa ugali, maana mboga zaja, safi sana Kapulya

ray njau said...

Duh!!Kilimo kwanza hadi Ughaibuni?

Salehe Msanda said...

Hongera.
Hii inaonyesha ni jinsi gani unaenze masuala ya kulima na kwa lengo la kupata vitu natural.
Pia inaonyesha ni jinsi gani unaenzi utajiri wetu watanzania. Kuwa na nchi yenye ardhi na mabonde ya kutosha kwa kilimo.
Kila la kheri

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki/Rachel,Kaka Sam, nyahbingi worrior, Ester, Kaka Ray, Dada P na Kaka Salehe Ahsanteni sana kwa mchango wenu. Vikiwa tayari sitakosa kuwakaribisheni wote wote wote...ila kama alivyosema Ester kuwa atakuja na unga maana hapa mahindi au mihogo inakataa.

simba deo said...

Hongera kwa sababu nyingi. Baadhi ni:
1. Kumiliki ardhi kama hiyo Ulaya
2. Kujishughulisha na shughuli za kilimo katika mazingira hayo
3. Kujali afya yako kwa kuushughulisha mwili
4. Kujali afya kwa kula vyakula kutoka bustanini kwako moja kwa moja
Lakini ... du ... usoni ... naona unawaza mbaaaali sana ... pengine Songea? Lakini hongera sana mdada.

Na Mpangala said...

Mlongo hii pitiku mi nitaifungia safari. safi sana mlongo inapendeza kwa kweli.