Tuesday, June 5, 2012

KWANINI PILIPILI MBUZI INAITWA HIVYO? NA JE KWA NINI HIKI CHOMBO ZA KUKUNIA NAZI PIA CHAITWA MBUZI?

Pilipili mbuzi zikiwa kwenye mti jee unajua kwanini zina itwa Pilipili Mbuzi? ni kwa kuwa zina faa sana kwenye supu ya Nyama ya Mbuzi au?
N ahap ni mbuzi mwenyewe , sioni kama kuna mfanano hapa...
 ...na hapa sasa ni kifaa cha kukunia nazi nacho kinaitwa MBUZI . Mara chache nimesikia wengine wakisema kikunio au je kuna jina jingine ambalo mimi sijawahi kulisikia...naamini kwa pamoja tutafika pahala pazuri. Mchana,jioni au sijui usiku mwema....KAPULYA4 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Mmmmmh swali zuri, ngoja tuwasubiri wanaojua zaidi ili tujifunze pamoja!!!
Asante da'Kadala

wenu Kachiki!!!

ray njau said...

@Rachael;
Hapa hakuna kungoja bali ni sema usikike.
Mbuzi ana fujo na kamwe hana utulivu kama pilipili zenyewe zinavyowasha na kukera.Ukaaji wa mbuzi akiamua kutulia na kutafakari hunyanyua shingo yake na kunyanyua kidogo miguu yake ya mbele na ile ya nyuma hubakia chini kwa kiasi fulani.Nahisi hapo ndiyo wa ubunifu.
Nawaza tu kwa sauti kubwaaaaaaaaa!!!

Mija Shija Sayi said...

@Ray Njau....Yaani umemaliza yoote!! Nakupa mia kwa mia, sikuwahi kufikiria hivyo kabisa.

Yasinta naona tumepata jibu..

ray njau said...

@Mija;
Thawadi yangu iko wapi?