Wednesday, June 13, 2012

WANAUME KATIKA MAPENZI NI KAMA MASOKWE...!

Ndugu zangu wapendwa leo ni JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA MAMBO /MAKALA,PICHA MBALIMBALI. Nale katika pitapita nimekutana na hii na si kwingine tena ni kwa  kaka yangu wa hiari Kaluse. KARIBUNI!!!!
Katika utafiti uliofanywa na akina Kruger na wenzake kwa wanyama jamii ya Sokwe, ilibainika kwamba kulikuwa na vifo vingi vya Sokwe madume wenye umri wa miaka 13. Hali hii ilitokana na sababu kwamba, kwa kawaida katika umri huo, Sokwe madume huwa wamefikia umri wa kupanda na kufanya mapenzi na hivyo huanza kushindana wenyewe kwa wenyewe wakigombea majike na hata kwa lengo la kudumisha hadhi yao miongoni mwa Sokwe wengine.
Katika hatua hii Sokwe hao hufikia mahali pa kupigana na hata kuuana kwa lengo la kujipatia wapenzi na kudumisha hadhi zao. Hali hii haiko kwa sokwe peke yao, bali hata kwa wanyama wengine pamoja na ndege wa aina mbalimbali.


Hata hivyo, pamoja na ukweli huo binadamu naye hajanusurika hata kidogo na purukushani za aina hiyo. Labda kinachomtofautisha binadamu na wanyama hao ni namna wanavyokabiliana na mashindano hayo. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, hata akichagua njia ya aina gani ili kushindana na binadamu wenzake, bado matokeo ya mwisho yatafanana na yale ya wanyama, yaani kifo.
Imeonekana wazi kwamba binadamu wa kiume ndiye mwenye mwelekeo mkubwa wa kupenda purukushani na kuhatarisha maisha yake. Ingawa binadamu huyu wa kiume au mwanaume hahitaji kupigana mweleka na mwanaume mwenzake ili kumpata mwanamke, lakini harakati zake ni zaidi ya kupigana mweleka.

Hata hivyo katika mazingira mengine, mieleka hupiganwa sana katika sura ya mieleka halisi au katika sura nyingine za ushindani wa kutafuta ushindi katika kumpata mwanamke. Wengi tunajua kuhusu habari za kuuawa kwa wanaume kutokana na vurugu za kugombea wanawake.

Tabia hii ya wanaume ya kuhatarisha maisha si ya leo, bali ni ya tangu kale. Huenda huko nyuma baadhi ya wanaume walitumia silaha kwa lengo la kuwadhulumu ama kuwauwa wanaume wenzao ili hatimaye waweze kuwamiliki wanawake wanaowapenda.
Kwa kawaida, wanaume hushindana wao kwa wao kwa lengo la kumiliki rasilimali na kuhifadhi au kudumisha hadhi na heshima yao ndani ya jamii wanamoishi.


Huu ndio ukweli wenyewe ambao hautofautiani hata chembe na ule wa Sokwe. Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali adimu kama vile fedha na anapoweza kusimika kwa uhakika heshima na hadhi yake, ndani ya jamii iliyomzunguka, mambo hayo humpatia thamani kubwa na kumrahisishia kazi ya kumpata mwanamke anayemtaka.
Au tu tumaliziae na ujumbe huu kutoka kwa CHOX FT ALIKIBA - TUSIGOMBANE

MUNGU AKIPENDA TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO NA RUDIO JINGINE. KWA SASA NASEMA JUMATANO NJEMA!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimesoma habari hii kwa kaka Kaluse nikawa mdomo wazi. Yaaani mtu mpaka anafikia kuua kwa ajili ya penzi. Jambo jingine nililojiuliza je? kama ni mwanaume anamuua mwanaume mwenzake kwa ajili yeye anamtaka mke wa wenzake, sasa hapa mwanamke anampenda nani? na je? ataishi kwa raha kwa yuli mume mpya? Mmmhh nimewaza kwa sauti...

ray njau said...

Hadithi inatufundisha nini wadau?
Wanaume tuache kuwa wababe katika familia na jamii yetu.

sam mbogo said...

Pia unajiuliza,kwanini mwanamke akimfumania mumewe anampiga au ana mdhuru yule mwanamke aliye mkuta na mumewe? badala ya kumpiga au kumtendea kituchochote mumewe amambaye kama ange sama no yasingetokea hayo.mara nyingi hii ni kwa wote wanawake na wanaume hufikiri yule aliye fumaniwa na mume/mke ndo mwenye kosa.wakati ukiangalia kwa undani sikweli mwenye kosa ni mumeo au mkeo kwani yeye ndiye aliye shindwa kusema noooo/hapana.kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! ulichosema ni kweli kabisa..
Kaka Sam! ni swali nzuri umeuliza ..nitajaribu kukujibu:- hapo inakuwa ni hasaira ni kweli kabisa hapo mwenye kosa si yule mwanamke alifumaniwa au mwanamume aliyefuniniwa bali ni yule aliyeanzisha. Lakini hapa pia inawezekana huwezi kujua nani kaanza..kwa vile mke kamfuma mumewe basi anapatwa na uchungu/hasira na kuanza kumpiga. ...Ila hapa napo ni pagumu kiduchu...

Rachel siwa Isaac said...

Mmmmhh dunia inamambo Waungwana, kaka s, Sam mwana wa Mbogo bisikuti ninakubaliana nawe kabisa, mimi pia huwa nawaza kwa nini nipigane/Upigane na mwanamke/Mwanaume eti kaniibia Mume/Mke wangu/Wako?
Kwani Amebakwa? nani kamsaliti mwenzie?

Asante kwa kutupatia Elimu hii Da'Kadala.

Wenu Kachiki.

Ester Ulaya said...

UBABE HAUNA MAANA KABISA, NI UKATILI DUH