Monday, June 4, 2012

WAZO LA JIONI YA LEO:- KUTOKA KWENYE TAIPURETA/typewriter MPAKA KWENYE KOMPYUTA/SIMU!!!

                                  
Leo nimekaa hapa nikawa nafikiri jinsi hali ilivyobadilika kwa haraka toka miaka ya 1990 mpaka leo. Nimekumbuka kazi yangu ya kwanza kama Karani pale Wilima Secondary. Nikiwa nachapa mitihani yote, kwa kutumia mashine/typewriter aina hii, na halafu kuburuza kwenye mashine ya kuburuzia ukitoka hapo nguo zote nyeusi.......Lakini leo
...mambo yamebadilika kweli.  Kuandika/kuburuza huhitaji kuchafuka ...nawaza kwa sauti na natamani leo ndio ingekuwa miaka ile...na hivi karibuni au nisema kwa sasa kila mtu ana simu na kila kitu kinafanyika kwenye simu...kaazi kwelikweli...

12 comments:

Mija Shija Sayi said...

Uninambie Yasinta kumbe wewe ni mtaalamu wa kuchapa bila kuangalia keyboard!! Hongera sana.

Kwa kweli mambo yanabadilika sana na huenda ndani ya miaka kumi ijayo mambo yanawezakuwa yamebadilika zaidi, labda hakutakuwa na kompyuta sampuli hizi..

Wako dada mkuu Mija.

Yasinta Ngonyani said...

Mija ndiyo mimi nimeifanya hiyo kazi...Ahsante sana..Si umeona zinavyoingia kwa kazi kompyuta na aina ya simu ambayo unaweza kuandika...Nimeitamani kazi yangu ...Hahahaaaa Dada mkuu haya dada wangu mkuu..

NN Mhango said...

Umenikumbusha kelele za taipuleta hasa kwa sisi wanoa kucha au waandishi wa habari. Kwa tuliosoma Afrika nadhani bado ule mchezo wa kuandika notisi na mitihani kwa mkono bado unaendelea. Nikiona huku power point inavyofanya kila kitu huku mwanafunzi akiandika kwa kompyuta naona wivu kusema ule ukweli. Umenikumbusha mbali Yacinta.

Simon Kitururu said...

Mmmmmmmh!

Yasinta Ngonyani said...

Mwal.Mhango..Yaani mwen yewe hapa nimepata hamu na nimekumbuka kweli enzi zile..maana vidole vilikuwa vinachapa kazi si mchezo...kumbukumbu za zamani ni nzuri sana.
Kaka mtakatifu Simon...Mbona mguno mrefu sana vipi?

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

ray njau said...

Hakika hizi ni zama za teknohama.Taipureta hususani ile ya manuali na baadae elektriki ni zilikuwa zana muhimu sana katika wetu wa huduma za uwakala wa forodha.Ilikuwa ni kaaazi kweli kweli.Lakini ilitusaidia sana kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa jasho na kujituma kuliko zama hizi za online kwa intaneti na tarakilishi[kompyuta] bila kusogeza miguu chini mufindi[kiyoyozi] kuanzia mwanzo wa kalenda hadi hitimisho la kalenda.
-----------------------
Mhubiri 1:1-11
------------------------------

1 Maneno ya mkutanishaji, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu. 2 “Ubatili mkubwa zaidi!” mkutanishaji amesema, “ubatili mkubwa zaidi! Kila kitu ni ubatili!” 3 Mwanadamu anapata faida gani katika kazi yake yote iliyo ngumu anayoifanya kwa bidii chini ya jua? 4 Kizazi kinaenda, kizazi kinakuja; lakini dunia inasimama mpaka wakati usio na kipimo. 5 Pia jua limechomoza, na kushuka, nalo linajitahidi kwa nguvu kwenda mahali pake ambapo litachomoza tena.

6 Upepo unaenda kusini, nao unazunguka kuelekea kaskazini. Unaendelea kuzungukazunguka sikuzote, nao unairudia mizunguko yake.

7 Mito yote ya wakati wa majira ya baridi kali inaenda baharini, hata hivyo bahari haijai. Mahali inapoenda mito hiyo ya majira ya baridi kali, hapo ndipo inarudi ili iende tena. 8 Mambo yote yanachosha; hakuna mtu anayeweza kuzungumza juu yake. Jicho halitosheki kuona, wala sikio halijai kwa sababu ya kusikia. 9 Lile ambalo limetokea, ndilo litakalotokea; na lile ambalo limefanywa, ndilo litakalofanywa; na kwa hiyo, hakuna jambo jipya chini ya jua. 10 Je, kuna lolote ambalo mtu anaweza kusema juu yake: “Ona hili; ni jipya”? Tayari limekuwako tangu wakati usio na kipimo. Jambo ambalo limetokea lilikuwako kabla ya wakati wetu. 11 Watu wa nyakati zilizopita hawakumbukwi, wala wale watakaokuja baadaye hawatakumbukwa. Nao pia hawatakumbukwa kati ya wale watakaokuja baadaye.

ray njau said...

Duh!!;wadau mjadala haujafungwa!

Anonymous said...

I have been surfing on-line greater than 3 hours these days, yet I never
discovered any fascinating article like yours. It's beautiful price enough for me. In my view, if all web owners and bloggers made excellent content material as you probably did, the net might be much more helpful than ever before.

Here is my homepage ... mouse click the following web site

Anonymous said...

If you would like to get a great deal from this post then you have to apply these strategies to your won weblog.


my web-site :: user talk:Ralfbucki - clasm
Also see my site - http://www.arabiaweb.com/user_detail.php?u=conniebole

Anonymous said...

Hi! Do you use Twitter? I'd like to follow you if that would be ok. I'm definitely enjoying your blog and look forward to new posts.


Also visit my web blog - related web-site

Anonymous said...

After exploring a number of the articles on your site, I
truly appreciate your technique of writing a blog. I saved
as a favorite it to my bookmark website list and will be checking back in the near future.
Take a look at my web site too and tell me your opinion.


Here is my blog post; 索引