Monday, June 4, 2012

KUTOKA SPORTSMAN MPAKA PORTSMAN...

Mimi si mvutaji wa sigara lakini naklumbuka nilipokuwa mdogo kulikuwa na sportsman zaidi na sigara nyingine nilikuwa natumwa kununu hasa mjomba wangu ani mvutaji sana wa sigara. Lakini mwaka jana nilipokuwa nyumbani katika pilikapilika nikaona kuna portsmn pia....ujazo, na kila kitu ni sawa ...mmmhhh labda sijui sigara zenyewe ni tafouti?.....MWANZO MWEMA WA JUMA!!!!

15 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

moja ni ya kenya nyingine ni ya bongo daslaam

Yasinta Ngonyani said...

Oh! kumbe sikujua hilo kwa vile zote nilinunu daslaam! Ahsante kwa taarifa..

Yasinta Ngonyani said...

Swali jingine kwa kaka Chacha au yeyete yule kwa nini wameandika "maden in Tanzania by Tanzania Cigarette Company Limited" kwa paketi zote mbili?

Ester Ulaya said...

ila siku hizi hakuna tena Sportsman, ndo ikaitwa PortsMan

Ester Ulaya said...

Ysinta ni zao la Tanzani, mimi nauza sigara siku hizi, ni made in here, wamebadilisha jina tuuuuu, siku hizi no Sportsman, na wakija wanataja sportsman mimi nawapa portsman wavutaji wanasema ni hizo hizo, jina tu ndo tofauti

Yasinta Ngonyani said...

Ester! Ahsante kwa mwelewesho.. Ndo maana huwa nasema kwenye wengi hapaharibiki neno..na pia kuuliza kunaleta majibu /kujifunza mengi. UKAPULYA:-)

ray njau said...

EPUKA MAMBO YANAYOMCHUKIZA YEHOVA MUNGU!!
=================================
Wanaume wawili wa genge Mwanamume na mwanamke wakinywa na kuvuta sigara Mwanamke akiiba

Uuaji.—Kutoka 20:13; 21:22, 23.
Ukosefu wa maadili.—Mambo ya Walawi 20:10, 13, 15, 16; Waroma 1:24, 26, 27, 32; 1 Wakorintho 6:9, 10.
Kuwasiliana na pepo.—Kumbukumbu la Torati 18:9-13; 1 Wakorintho 10:21, 22; Wagalatia 5:20, 21.
Kuabudu sanamu.—1 Wakorintho 10:14.
Ulevi.—1 Wakorintho 5:11.
Kuiba.—Mambo ya Walawi 6:2, 4; Waefeso 4:28.
Kusema uwongo.—Methali 6:16, 19; Wakolosai 3:9; Ufunuo 22:15.
Pupa.—1 Wakorintho 5:11.
Jeuri.—Zaburi 11:5; Methali 22:24, 25; Malaki 2:16; Wagalatia 5:20.
Maneno yasiyofaa.—Mambo ya Walawi 19:16; Waefeso 5:4; Wakolosai 3:8.
Kuitumia damu isivyofaa.—Mwanzo 9:4; Matendo 15:20, 28, 29.
Kukataa kuiandalia familia.—1 Timotheo 5:8.
Kushiriki katika vita au katika mizozo ya kisiasa ya ulimwengu huu.—Isaya 2:4; Yohana 6:15; 17:16.
===================================
Kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya.—Marko 15:23; 2 Wakorintho 7:1.
=================================

ray njau said...

Nchini China idadi ya watu wanaopata madhara kutokana na uvutaji wa sigara usio wa moja kwa moja imezidi milioni 740
(GMT+08:00) 2012-05-31 18:22:39
===================================
Madhara ya uvutaji wa sigara ni moja ya matatizo makubwa zaidi kuhusu afya ya umma, na tatizo hilo ni kubwa zaidi nchini China. Wizara ya afya ya China leo tarehe 31 imetoa ripoti ya kwanza kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara dhidi ya afya za watu.

Ripoti hiyo imefafanua madhara yatokanayo na uvutaji wa sigara na uvutaji usio wa moja kwa moja, pia imejulisha mbinu na hatua za kuacha uvutaji wa sigara. Ripoti hiyo imeonesha kuwa, nchini China idadi ya wavutaji sigara imefikia milioni 300, na wengine wapatao milioni 720 wanapata madhara kutokana na uvutaji wa sigara usio wa moja kwa moja. Takwimu zimeonesha kuwa, watu wapatao zaidi ya robo tatu hawaelewi sana madhara ya uvutaji wa sigara kwa afya, na watu wapatao theluthi mbili hawaelewi madhara kutokana na uvutaji wa sigara usio wa moja kwa moja.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa, China ni nchi inayozalisha sigara kwa wingi zaidi na kutumia sigara kwa wingi zaidi kuliko nchi nyingine duniani, kila mwaka idadi ya watu wanaokufa kutokana na magonjwa yanayotokana na uvutaji wa sigara imezidi milioni moja, na kama haitadhibiti hali ya uvutaji wa sigara kote nchini, ifikapo mwaka 2050, idadi ya vifo itazidi milioni 3.

Kauli mbiu ya siku ya dunia isiyo na tumbaku mwaka huu ni "shughuli za uzalishaji wa tumbaku zinavyosumbua kazi ya udhibiti wa tumbaku", na mwito wa siku hiyo ni "mapambano kati ya maisha na tumbaku". Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, mjumbe wa Shirika la afya duniani nchini China Bw. Michael O'Leary amedhihirisha kuwa, tumbaku inasababisha vifo vya watu milioni 6 kote duniani, na kuleta hasara ya kiuchumi ya mabilioni ya dola za kimarekani.

Mwaka 2003 serikali ya China ilisaini "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku" wa Shirika la afya duniani. Kuanzia mwezi Mei mwaka jana, China imetekeleza rasmi kanuni ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya majengo ya umma. Aidha, China imeandika kanuni kuhusu "kutekeleza kwa pande zote marufuku ya uvutaji wa sigara ndani ya majengo ya umma" kwenye mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano, na kuweka mpango halisi na ratiba ya kazi ya udhibiti wa tumbaku. Hata hivyo, waziri wa afya wa China Bw. Chen Zhu alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema, China bado inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya udhibiti wa tumbaku. Akisema:

"Katika miaka ya hivi karibuni, uzalishaji wa sigara bado unaongezeka, madhara ya tumbaku yanaongezeka bila kupungua, hasa umma bado hawajaelewa ipasavyo madhara ya uvutaji wa sigara, na viwanda na kampuni za tumbaku bado zinatembeza mbinu zao, kama matatizo hayo yote hayataweza kutatuliwa, basi suala la udhibiti wa tumbaku halitaweza kutatuliwa kihalisi."

Waziri huyo amesema, katika siku zijazo idara za afya zitaimarisha zaidi kazi ya udhibiti wa tumbaku, huku zikifanya juhudi za kueneza ujuzi kwa umma kuhusu madhara ya tumbaku kwa afya za watu, ili kuongeza uelewa wa watu wote katika jamii kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara.
===================================
Webradio
Sauti
2:00-3:00 asubuhi
Kipindi cha leo Kipindi cha jana
6:00-7:00 adhuhuri
Kipindi cha leo Kipindi cha jana
2:00-4:00 usiku
Kipindi cha leo Kipindi cha jana
Dira ya usikilizaji
Maoni yako
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved.
16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040

nyahbingi worrior. said...

Sigarate smocking is dangerous so ligalize it and i man will advertis it.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray..Ahsante

Kaka nyahbingi worrior.. nakubaliana nawekabisa..halafu unajua watu sijui tupoje yaani hapo kwenye paketi wameandika kabisa ONYO:- UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO. Lakini hata hivyo haiwatishi watu...kaaazi kwelikwwli

John Mwaipopo said...

rais mmoja wa zamani afrika aliwahi kunukuliwa akisema "if you smke cigarettes you smell like a man". marais kibao wanavuta sigara sijui hawaogopi hatari hiyo?

ray njau said...

Kuendelea na mada hii ni kujiingiza katika matangazo ya biashara bila ridhaa ya wenyewe wala malipo.Kumbuka kuwa bajeti ya kutangaza ubora wa bidhaa hii ni kubwa labda zaidi ya mara elfu moja dhidi ya ile kutangaza madhara yake kwa jamii.Hapa kibarazani tupo kwa ajili kutangaza ubora wa bidhaa hii au madhara yake kwa jamii?Kwa hapa tupo kijamii zaidi acha nihitimishe kwa hivi:ONYO:- UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YA JAMII YETU.!!

Mija Shija Sayi said...

Uvutaji wa sigara ni hatari, ulimaji wa tumbaku je??

Nawaza tu kwa sauti.

Ester Ulaya said...

na walimaji wa tumbaku hadi wanapewa pembejeo, Da'Mija

ray njau said...

@Mija/Ester;
Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kupanga.Nasikia Nguruwe na uchafu wake wote kamwe hatafuni tumbaku!
Kamwe afya ya mwanadamu haiwekwi rehani.
Ni wazo tu wadau wenzangu na endeleeni mada kwa kuwa uhuru wangu unaishia pale uhuru wako unapoanzia.