Wednesday, April 2, 2014

MAMA MJASIRIAMALI..ANAPIKA POMBE

 Mama huyo hayupo nyumba katika kutaka kuitunza familia hapa anapika pombe. Kupika pombe ni kazi kubwa kwa kweli kwanza maandalizi yake ni makubwa halafu kuungua moto. Pia kupata kipato inategemea hiyo pombe "inoge" iwe nzuri. Nimewahi kutazamia jinsi inavyopikwa hii pombe wakati mama akipika hasa ile ya mihogo MYAKAYA si mnajua kila pombe huwa na jina lake baadhi ni kama vile kindi /komoni pombe ya mahindi Mbege pombe ya ndizi. Na pia pombe  si ni kinywaji tu cha kujifurahisha au kupata uchumi, kwa kifupi hasa sisi WANGONI kwa asili hupenda sana kunywa maji wakati akila chakula ila baada ya chakula hupenda kupata pombe/ugimbi kidogo kushushia ugali/chakula. Pia pombe huweza kuwashirikisha watu kwa kufanya kazi pamoja, kama vile kulima/kuvuna, kwenda kilabuni,  pombe ya harusi, na pombe ya sadaka. Na kwa kawaida huwa mtu/watu maalumu ambao huja mapema alfajiri kuonja kama pombe ipo safi "imenoga" kabla haijachunjwa na kwenda kilabuni au kunywewa.
Hapa naona ni ile POMBE ya kilabuni. Huyu baba kaona anachelewa kaamua kuchukua ndoa nzima  ameona "dumla" au kisonjo wangoni wanaita KIJOMELA. Nitawaonyesha siku yake. Kwa leo tuishia hapa. ANGALIZO:- TUSISAHAU SASA NI KWARESMA TUSINYWE KUPITA KIASI POMBE SI MAJI. Kapulya.

3 comments:

NN Mhango said...

Hii kitu noma sana don't touch especially mwambie shem aiogope kama ukimwi kwani inaua kila kitu.

Yasinta Ngonyani said...

Hahaaa Kaka Mhango...unasema wasiguse wakati wenzako ndo wanashinda na kuamkia hapo...Ila duh ama kweli huu ni ubunifu wa pekee kutengeneza kitu mpaka kumfanya mtu alewe...mmmmhhhhh..shem wako nadhani hii anaiotea mbali...

Bashikulu Mligo said...

Nampenda huyo mama mjasiriamali anahangaika na maisha yake na watoto.
Lakini hebu tafakari hii, Huko makanisani (ukiacha wakatoiki) akina
mama wanaopika pombe wanonekana wanatenda dhambi ya kuandaa kilevi,
wanatengwa hata sakramenti. Umewahi kujiuliza kwamba watu wanaofanya
kazi kwenye viwanda vya bia mbona hawatengwi. Huyo mama na wafanyakazi
wa kiwanda cha bia wote wanatengeneza pombe. tafakari.