Monday, April 21, 2014

NI JUMATATU YA PASAKA:- NA TUSALI SALA HII YA FAMILIA KWA PAMOJA...MAANA SISI SOTE NI FAMILIA MOJA!!!

Milango imefungwa, Ee Bwana,
Yule mtoto mchanga amelala,tunajisikia salama,
Tuna raha ya ndani, kwani tumeshiba,chakula kilikuwa kizuri,
Kinatuletea faraja.

Huu ndio wakati wa kukugeukia, mwishoni mwa siku hii ya leo,
Kama familia - familia yako, ambapo Kristu anaishi.

Mwa ajili yetu, kila mmoja wetu, Bwana, tunakushukuru. Kwa ajili ya siku hii ya leo.
Iliyojaa mambo mengi, mema na yasiyo mema sana. Kwa yote tunakushukuru.

Tunapoangalia nyuma, mara ngingine, ni rahisi kuona kwamba ingewezekana kuwa vizuri zaidi.
Hapa na pale, tumeshindwa kukupendeza, kwa neno la hasira. Na lile ambalo hatukulitimiza.

Tunasikitika, Bwana tusamehe. Kwani tunahitaji upendo wako. Tunakuhitaji wewe, ukae nasi usiku  huu wa leo. Ili kutulinda, kutubariki, kwani wewe ndiwe kuta za kweli na paa za nyumba  zetu.
Utubariki tulalapo, utujalie ndoto zetu ziwe za furaha. Na utujalie tuamke kesho tukiwa na uzima mpya tele, nguvu mpya, na starehe mpya. Ili tuweze kuishi tena siku nyingine. Amina.

2 comments:

Anonymous said...

Nakutakia wewe na familia yako Pasaka njema. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Salumu..Nina imani nawe Pasaka yake imekuwa njema na inaishia kwema!