Tuesday, April 15, 2014

KWA NINI URAIA WA NCHI MBILI?

Mara nyingi sana nimekuwa nikujiuliza hili swali na pia nimekuwa nikisikia ya kwamba itatokea na kwamba swala hili lipo jikoni yaani BUNGENI lakini hakuna kinachotokea. Sijui kama kuna Mtanzania ambaye anapenda kuwa raia wa nchi nyingine kuliko nchi aliyozaliwa. Naamini kabisa kama Mtanzania  ya kwamba HAKUNA MTANZANIA ASIYE  IPENDA TANZANIA NCHI YETU. KATIKA TEMBEA TEMBEA NIMEKUTANA NA HII EBU UNGANA  NAMI  KUMSOMA KAKA Peter H.A. Owino KARIBUNI PIA NAKUMBUKA NILIWAHI KUANDIKA/KUDODOSA  BONYEZA http://ruhuwiko.blogspot.se/2009/10/uraia-wa-nchi-mbili.htmlKUJIKUMBUSHA
Tanzania na Diaspora.

Wakati watanzania tunaendelea kushuhudia kikao cha marekebishia ya Katiba kikiendelea napenda kujumuika na baadhi ya waliopata nafasi kuchangia kuhusu swala la uwezekano wa uraia wa nchi mbili (Due citizenship).
Katika ya nchi yetu tuipendayo kwa sasa haitambui uraia wa nchi mbili, kwa maana kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine unapoteza haki ya kama raia wa Tanzania, Swala hili linapaswa kuangaliwa kwa makini wakati huu wa marekebisho ya katiba, Kwa maoni yangu iwe ruksa kwa Mtanzania kuwa na uraia wa Tanzania hata kama utakuwa umechukua uraia wan chi nyingine, swala hili lisipoangaliwa makani ama likiangaliwa haraka haraka linaweza tafsiriwa kuwa watanzania hao wanatamaa ya kutaka huku na kule, si sahii kulitafsiri namna lightly namna hiyo, wengi wa watanzania waliokwenda kuishi kasha kuombauraia kuishi nchi nyingine hawakuwa na maana wa kuukana Utanzania na ukiangalia mpaka sasa hakuna anayetamba ama kuupondda U-Tanzania popote alipo.
Wengi wa watanzania wanaoishi ughaibuni ama nchi yoyote nje ya Tanzania na kupata uraia wa nchi hiyo bado wanajitambulisha kama watanzania, uraia wanaopewa ni haki ambayo wengi wao wameifanyia kazi muda mrefu sana katika nchi waliyopo, na ili kupata baadhi ya haki muhimu inabidi watambulike kama raia, kwa maana hiyo inabidi kuomba uraia wan chi waliyopo, lakini hii haimaanishi hata kidogo kuwa sasa Tanzania basi. Hata watanzania waliokuwa wakubwa kisiasa waliishi nje lakini inafika wakati wanarudi nyumbani kama kina Abrahaman Babu na Mzee Kambona nyumbani ni nyumbani huna ujanja.
Watanzania hao amabao baada ya kupata uraia wa nchi wanayoishi sasa wanatakiwa kuomba visa kuingia Tanzania, yani Mswahili wa Tarime au Ndanda sasa wanakuja Tanzania kama mgeni!, wanalipishwa kiingilio kwa dola katika mipaka yote ya Tanzania. Kuwapa haki katika nchi yao mama (Tanzania) ni swala muhimu katika kuendeleza Tanzania pia, maana yangu ni kuwa wengi wanafanya kazi nje ya nchi lakini mawazo yao ni Tanzania wengi ama wote wanandugu ambao bado wanawasiliana nao kila mara, katika kuwasiliana huko wengi wanawekeza Tanzania sababu ndio kwao na ndipo siku wakikata kauli wengi watarudishwa na kulazwa walipolala ndugu zao wengine.
Raia wengi tunajua ugumu wa Maisha yaliyopo Tanzania tuna wahitimu wengi ambao wanamaliza na kufaulu vizuri bila kupata ajira, wapo wenye bahati ambao humaliza na kuanza kazi moja kwa moja lakini wengi hawana bahati hiyo. Mtanzania ambaye amekwenda kujiendeleza nje analiona hili swala na anajua labda hayupo kwenye kundi la wenye bahati kwa maana kuwa atarudi nyumbani na hakuna ajira na wanaopata ajira wengi kama walimu wanaanzia mshahara wa shilingi 277,00=, kiasi ambacho ambacho ukijiuliza mwalimu huyu ambaye amepanga na kutumia public transport anafikaje mwisho wa mwezi hupati jibu, ukipata bahati unaweza anzia taasisi zinazolipa 750,000= kwa mwezi, lakini ni watanzania wangapi wanabahati hiyo?.
Nchi kama Uholanzi mshahara wa mwezi unaanzia Euro 1440 sawa Tsh 3,240,000 Norway wanaanzia euro 2000 na Uingereza ni zaidi ya hapo, kwa haraka haraka watu hawa wanaweza kuishi kwa amani huko walipo nabado wakasaidia ndugu zao ambao wapo Tanzania.
 
Nchi kama uingereza ukiwa raia una haki kuishi kwa kutegemea Serekali kwa chakula malazi ,matibabu yaani hata kama hufanyi kazi, kwa maana hiyo Mtanzania huyu akipata kazi na anaishi nchi ambayo kwa kawaida huwezi kujinunulia kiwanja na kujenga unless uwe Millionea siku zote atakuwa na mawazo ya kuja kuijenga nyumba yake nyumbani na ya kisasa kama anayoiona huko nje, na kwa vile anaishi nje basi hii nyumba yake wataishi watanzania ambao kama walivyo wengi wetu hawana uwezo wa kujenga kwa haraka na kwa mishahara halali. Tutakaporuhusu Mtanzania anayepata uraia nje kuendelea na uraia wake wa Tanzania kama atapenda basi ataendelea kulala na kuwaza Tanzania.
Mimi nimeishi nje ya Tanzania kwa muda sasa kwahiyo naelewa umuhimu wa kuendelea kuwa raia wa Tanzania, naelewa umuhimu wa siku moja kuja zikwa pale walipozikwa ndugu zangu.
Wajumbe wa Bunge wa katiba watumie busara katika kujadili hili swala bila kusahau kuwa watanzania wanaoishi je na wamepewa uraia huko wanapenda kuendelea kuwa watanzania, wajumbe watakuwa wametenda jema kuruhusu uraia wa nchi mbili hasa kwa watanzania waliobahatika kupata uraia wa nchi nyingine katika njia ya kutafuta maisha kwa ajili yao wenyewe na ndugu zao.
Sababu nchi nyingi wanazoishi Wazanzania nje ya Tanzania system yao ya kufanya kazi ni 100% kazi hivyo watanzania wengi wanajifunza na kunakili mifumo hiyo ili siku wakirudi nyumbani wawaambukize watanzania wenzao maana nchi nyingi za nje unaposema kazi unamaaninisha kazi na si kazi ya kuingia saa unayotaka na kusign na kuondoka, unakula kwa jasho lako kihalali na ukijituma unapata, Japo ni kidogo lakini watanzania walio nje wanaweza na wamekuwa wakichangia kihalali kidogo walicho nacho katika kuendeleza uchumi wa Tanzania wengi wakati wa mapumziko huja Tanzania na wengi wao hawaji mikono mitupo ama hawaji kutengemea ndugu za walioko Tanzania badala yake huja wamekamilika na vitu ambayo wengi huvituma bandarini na kulipia ushuru, siku wakiwa wanaondoka kurudi makazini wengi wao huondoka watupu na kuanza upya katika arakati za kukusanya ili akirudi tena Tanzania aendelee pale alipoachia mara ya mwisho.
Mtanzania anayeishi nje hana sehemu ya kuishi kwa furaha zaidi ya Tanzania, hana sehemu anayoishi kwa amani zaidi ya Tazania, Mtanzani huyu hana sehemu aliyo na marafiki wengi zaidi ya Tanzania, Mtanzania huyo ambaye wazazi na ndugu zake wote wako Tanzania leo anaadhibiwa kwa kitendo cha kwenda kutafuta kipato ambacho hakipereki popote bali Tanzania.
 
Miaka ya sabini ilikuwa inaeleweka pale alipoadhibiwa mtanzania aliyekwenda kusoma Urusi, Denmak, Hungary na akakataa kurudi, sababu tuliitaji wataalam wetu ambao hatukuwa nao wa kutosha na wengi wao waliperekwa na gharama za serekali, Zanzibar tulikuwa na chuo kimoja tu tena cha ualimu pekee na sasa kuna vyuo zaidi ya vitatu vikubwa,bara kulikuwa na
chuo kikuu kimoja tukilicho kuwa kinahitimisha wanafunzi 15 tu na sasa tunavyuo zaidi ya 30 wanaohitimu ni zaidi ya 110,000 kwa mwaka, kwa miaka hii wengi wako nje kwa gharama zao katika kutafuta kilicho bora kwa ajili ya watanzania wenzao na sasa akifanikiwa kupewa uraia na nchi husika ili aishi kwa amani na haki zote za kufanya kazi kusoma nk Tanzania inamwambia sasa hapa ni wewe ni mgeni ukija kumuona mama ama baba yako ama kuendeleza nyumba yako unayojenga kijijini kwenu kule Butiama basi lipa kiingilio (visa)!!.
Watanzania walioko nje hawako nje sababu hawaipendi Tanzania na anafikiria hiyo atakuwa anajidanganya, Tanzania iko miyoni mwetu na hata serikali ingeweza hata ingeruhusu tukatengeneza system ya kupiga kura wakati chaguzi kuu zinapowadia. Wawakilishi wa vyama vya siasa katika bunge hili lililopewa heshima ya kurekebisha katiba tunawaomba kuingiza swala hili katka katiba mpya, Mheshimiwa Membe amekuwa akisikiliza na kwa makini kilio hiki cha watanzania walioko nje, pia mheshimiwa Kikwete amekuwa akikumbana na hili ombi kila wakati akikutana na watanzania waishio nje, katika kikao chake cha mwisho na watanzania Uingereza pale Wembley Mheshimiwa Raisi alisema swala hili limeingizwa kwenye rasimu kwahiyo liko ndani ya bunge kujadiliwa, napenda kumpongeza Mh Dr Kikwete kwa kutambua kilio hicho mpaka kumteua Singo kuwakilisha diaspora (thank you Mr President) katika kikao hicho.
Lakini sababu kwa walio wengi swala hili si muhimu kwao huko bungeni tunaomba mfungue macho na kulipa umuhimu. mnapojadili mjue mnamuongelea Masatu, Juma, Asha, Owino, Yasunta na wengi ambao huko waliko japo wamepewa uraia lakini wanahesabiwa kama wageni hawatakubalika kama wenyeji unless wameishi zaidi ya miaka 30, mjue mnamjadili mtu ambaye anakuja Tanzania sio kuchuma ama kujifunza Kiswahili na mila za Tanzania la hasha mnajadili maisha ya mtu amabaye amewaachia watanzania wenzake nafasi za ajira Dar , Mwanza ama Ndada na kwenda kutafuta huko nje ya nchi na anachopata japo kidogo lakini anakula na wakwao –WA-TANZANIA.
 
Mungu bariki Tanzania yetu.
Peter H.A. Owino
Rorya
Tanzania.
Live in UK
Nami nasema tena na tena MUNGU IBARIKI SANA TANZANIA YETU. PAMOJA DAIMA!!!

4 comments:

Anonymous said...

Peter Owino kaeleza kwa lugha nzuri sana Na ambayo kila mtanzania itamgusa,wajumbe waache wivu wa kijinga wapige kura ya yes to urai. pacha, kuhamia nchi nyingine isiwe dhambi Ni kikazi tu nd wajumbe.


Ommy.

NN Mhango said...

Mie wala huwa hawanihangaishi zaidi ya kuwasuta unafiki. Wameruhusu wahindi na vigogo kuwa nao uraia pacha lakini sisi wanatukatalia. Kwa wale wanaoona kama wamenyimwa tonge wajaribu kujiuliza ni vijana wangapi wa Kitanzania wanatamani kuzaliwa paka Ulaya. Mie siombi wala kumbembeleza. Uraia pacha ni haki yangu na hakuna anayeweza kuizuia na akifanya hivyo ni kwa muda tu. Kinachokera ni pale wale wale wanaotukatalia uraia pacha kutwambia eti tukawekeze nyumbani. Wanashindwa kututofautisha na makada wa CCM waliotamalaki ughaibuni wakisota kiasi cha kujigonga kwa CCM. Je hawa wanaweza kuwekeza Tanzania zaidi ya kujikomba kwa CCM ili wapate namna ya kurudi nyumbani kiulaini baada ya kushindwa kufurukuta huku ughaibuni? Usomi na nafasi yangu hapa ughaibuni wala sibembelezi nyani wala kenge. Siku ikifika ya kutoa uraia pacha watatoa watake wasitake. Ukiona vipi unaingia kule kama TX na kuwaliza. Hivyo nawashauri wenye uchungu na nchi yetu someni kwa sana tena fani kali kali mtarejea kule na kulakiwa kama wafalme. Mfano washaurini vijana wenu wasomee masuala ya gesi na mafuta muoni au mambo ya idadi ya watu na uchumi wa kisasa.

Anonymous said...

Kazi kwa wajumbe wa Bunge la kurekebisha Katiba.

Anonymous said...

please bring uraia pacha as Peter Owino analysed.

Said