Monday, April 21, 2014

BUSTANI YETU:- LEO MAMBO YAMEPAMBA MOTO MTU NA JEMBE....

 Ukiwa na shamba lazima uwe na jembe leo ni kukatua/kulima maana mikono imewasha kweli ...Kutoka tu mazoezini nikazamia bustanini  kama muonavyo:-)
 Hapo sasa jembe linainuka kwa "nguvu" kweli
 Kama muonavyo ukilima/katua lazima kutoa nyasi...na hapo kwa mbali unaona ni vitunguu saumu nilipanda mwaka jana na sasa ni vikubwa.  ....leo tayari nimepanda/atika mchicha, mboga maboga, figiri, vitunguu,  pilipili hoho  pia nyanya.
Kapulya ana alikuwa na msitu kwa hiyo sasa ni mavuno ..kuni hizo ..ukitaka kununua karibu:-)
Hivi ndivyo ilivyokuwa  siku yangu kwa leo na sasa napumzika kidogo kwa kikombe cha CHAI.  Majembe yapo mengi karibuni:-)

4 comments:

Anonymous said...

Nakuona Dada Yasinta, na jembe lako, mkulima mwenye shamba haswa! Haya pongezi kwa kuanza kutuandalia shamba tayari, mie nasubiria sana na kwa hamu hayo mazao na siku ya kuvuna niite nije kukusaidia ili vingine nibebe. Siku njema.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu! Nakwambia jembe leo nimenoga si mchezo... Ahsante kwa pongezi umeniongezea moyo. Hakuna shida si huwa wanasema mkulima mmoja walaji ni wengi...nitakuita na utavuna tani yako:-) nawe uwe na siku njema sana.

Bashikulu Mligo said...

Hongera! kumbe na huko Ulaya mnalima.

Anonymous said...

Kilimo kwanza unakumbukia ruhuwiko nn shem? Haya bwana uwe na siku njema. MSHANA