Wednesday, April 16, 2014

HII SIJUI IMEKAAJE? AU NDIYO MAANDALIZI YA PASAKA????

KITOWEO CHA PASAKA
Inaonekana mnyama/mbuzi beberu anakula mgumo hapo lakini akina baba hawakubali kushindwa. Je wewe nawe umejiandaa PASAKA hii na beberu? au labda kondoo....mmmmhhh,,, msije kujisahau IJUMAA KUU   hakuna kula nyama!...
Ila mimi nikipata mlo kama huu nitaridhika kabisa kabisa..Ugali, mlenda/bamia na samaki.
NAWATAKIENI SIKU NJEMA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-) KAPULYA.

5 comments:

NN Mhango said...

Da Yacinta unauliza swali badala ya kuuliza jibu! Ngoja nikupe jibu. Sijui hii nayo imekaaje? Napita tu nikikutakia pasaka njema. Je umekumbuka kufunga hasa kula nyama? Blessed be.

rafikio wa hiari said...

rafiki huu mlo kesho unahusika sana...nikishapika nitakutumia picha walu ule tena kwa macho!

Yasinta Ngonyani said...

kaka Mhango! Mmmmhh, si unajua Kapulya...Haya Ahsante kupita hapa nawe PASAKA IWE NJEMA SANA NA FAMILIA. NINA HAKIKA BARIDI IMEPUNGUA SASA:-)
Rafiki wa mimi! yaani kweli kabisa na hapa ni huo mlenda tu ndo zaidi maana samaki ina damu..ila ntafurahi sana kupata hiyo picha na kula kwa macho.

John Mwaipopo said...

samaki si nyama?

Yasinta Ngonyani said...

kaka John! Nimependa swali lako ni kweli samaki pia ni nyama ila ni tofauti na ndio maana twasema nyama ya ngómbe na samaki ni samaki ila vyote vyatoa damu.