Tuesday, April 8, 2014

TUDUMISHE UTAMADUNI WETU...HAPA NI BAADHI YA VIFAA VILIVYOTUMIKA SANA HAPO KALE NA PIA BADO VYATUMIKA

Kama mila na desturi zisemavyo usisahau ulikotoka na uendapo sehemu chukua na vile vyombo ambavyo ni asili yako. Hata kama hutatumia lakini unaweza kuwaelezea wanao wapi unatoka. Fuatana nami kuona baadhi ya vyombo asili nilivyochagua leo....Pia naomba msaada kama kuna anayejua majina ya kiswahili baadhi ya hivi vifaa.
 
 Hapa ni vifaa ambavyo huitwa VISONJO (ungonini tunaita VIJOMELA) hutengenezwa kwa majani ambayo huota ovyo ovyo tu (kingoni tunasema MALULU) anayejua kiswahili naomba msaada. Kifaa hiki ni maalumu kwa kunywea pombe hasa pombe ya kienyeji kama myakaya, komoni pia hata togwa badala ya kikombe;glasi au hizi waitazo dumla/robo nk.
 Hapa ni kifaa ambacho ni kwa kuhifadhia nafaka, kuwekea pombe nk..ni aina ya kikapu na miguu minne. Sisi wangoni huita (LINDANDALI). Kimetengenezwa kwa miazi na miti.
 Kwa nini kutumia chujio za kisasa ambapo zipo kama hizi. Mimi natumia hizi zinachunja sana kabisa nazi, na karibu kila kitu nitakacho kuchunja....ila nimekosa ya kuchujia chai.:-(.
Na hapa ni ungo mdogo ambao  hutumika sana katika nyumba nyingi sana Afrika/Tanzania. Ila sisi wangoni tuna jina letu tunaita (CHIHENEKO). Hiki waweza pia kupakulia/kuwekea ugali yaani kama sahani.

2 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Hakika dada wa mimi KADALA, Wewe ni mwanamke kwa kweli.....Hongera sana.

Yasinta Ngonyani said...

Dada KACHIKI! DUH! Bonge la wasifa ahsante sana. Si unajua nyumbani ni nyumbani