Saturday, April 12, 2014

MAUA MAZURI YAPENDEZA...NAPENDA SANA MAUA NIMEPATA HILI KAMA ZAWADI NA....:-)

NIKAONA NILIIMBIE NA HUU WIMBO TULIOKUWA TUKIIMBA ENZI ZILEEEE je nawe unakumbuka kama hukumbuki basi ni hivi kuimba!!!
1. Maua mazuri yapendeza x 2
    Ukiyatazama utachekelea
    Hakuna mmoja asiyeyapenda x 2

Kwa kutaka kuimba bila kukosea basi fuata hii hapa:-)
 Au pia tusiwasahau na watoto, si mnakumbuka na huu wimbo  haya wazazi waimbieni watoto wenu  kwa raha zote ni kama vile umsomeapo/msimuliapo hadithi :-
2.Mtoto msafi apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyependeza x 2
 
3. Mtoto mtii apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyempenda x 2

JUMAMOSI IWE YENYE UPENDO, FURAHA  JUU YA KICHEKO. SI MNAJUA KUCHEKA/KICHEKO NI DAWA ISIYOLETA MADHARA.
KUMBUKENI TUPO PAMOJA!!


8 comments:

Anonymous said...

Nimeipenda post ya leo, mauaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteeeeeeeeee....mimi pia ni mpenzi mno wa maua

Manka said...

Nimependa sana rangi ya hilo ua,umenikumbusha mbali sana na hizo nyimbo,weekend njema Dada yangu

Yasinta Ngonyani said...

Dada Manka....yaani hata mie hiyo rangi nimeipenda si kawaida ua la bluu. Ni furaha kwangukana umepata kumbukumbu.....naamini nawe utakuwa na weekend njema.

Anonymous said...

jamani rafiki umenikumbusha mama yangu (may her soul rest in peace) alikua anapenda sana maua, its a shame sisi watoto wake hakuna aliyerithi hili la upenzi wa maua...
Mimi nimekua kwenye mazingira ya kuzungukwa na maua si ndani wala nje ya nyumba, vurugu tupu! Tukisafiri airudi huko lazima amebeba ua jipya!

Anonymous said...

nimesahau kuweka jina hapo juu, ila ni mimi rafikio....

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki yangu....si watoto wate hywa wanarithi wazazi walivyo. Huna haja ya kuona aibu inawezekana umerithi kitu kingine. Mama anakuelewa.

rafikio wa hiari said...

nakubaliana na wewe rafiki