Sunday, April 6, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI JIONI/JUMAPILI NJEMA SANA WOTE...ZILIPENDWA/NA MITINDO YAKE!!!

 zilipendwa 27/4/2009
Nimependa sana mkoba huu maana unamechisha na nguo yangu hapo juu. Ilikuwa ni hivi tu kwa JIONI HII YA JUMAPILI HII na NINAPENDA KUWATAKIENI WOTE JIONI /MCHANA/ASUBUHI NJEMA YA SIKU/JUMAPILI HII.

7 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana KADALA wa mimi...Iwenjema kwako na familia pia....

Mkoba mzuri sana na huyo Mrembo juu hapo katokelezea,Jee akiongezea na huo Mkobaaaa..uwiiiiiiiiiiii.

Mingi Love kutoka kwa KACHIKI.

Nicky Mwangoka said...

Haya sasa kinadada muache kupendeza tena. Simple but pretty

Manka said...

Dada Yasinta umependeza na hiyo rangi imetuliaa na hiyo pochi yaani itakuwa mmechicho wa nguvu...Nakutakia wiki njema

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI! Jumapili kwa kweli ilikuwa njema ingawa iliishia mzigoni....Yaani huu mkoba nimeupenda mno ila duh! mtu huwezi kupata vyote.
Kaka Nicky! Nitafuata ushauri wako:-)
Ndugu wa mimi Manka! Ahsante alo yaani ni kweli kabisa hii rangi ni bomba sana naipenda sana. Nawe uwe na mwanzo mwema wa wiki:-)

Mija Shija Sayi said...

Yasinta raha jipe mwenyewe banaa..utafute mkoba ufurahi na roho yako...

Hata mimi nimeupenda kusema kweli.

rafikio wa hiari said...

niliachia comment yangu hapa rafiki mbona siioni?
Anyways nilichokwambia nikwamba hii pochi usiiachie itaendana sana na viwalo vyako vyeupe unavyopendeleaga kutinga!

Yasinta Ngonyani said...

Dada mkuu msaidizi..ndo naisaka ...ila nikiikosa si kitu:-(

Rafiki yangu wa hiari. ....nitaitafuta we ngoja tu..umenicgekesha eti "viwalo vyako vyeupe unavyopendekeaga kutinga"..mwisho wa nukuuu. Ni vyepi hivyo?