Friday, April 11, 2014

MAMBO YA BUSTANI YANANUKIA NUKIA :-) TUMALIZE JIONI HII YA LEO KIHIVI UKULIMA!!!

Hii ni ile BUSTANI yetu, nilikuwa kimyaaaa, nilikuwa natifuatifua. Karibuni tu kutakuwa na zile mbogamboga na viungo. Hivyo vionekanavyo hapo ni vitunguu saumu. Nilipata ushauri kuwa ukipata mwezi wa kumi mapema mwanzoni mwa mwaka au kama baridi imepungua huchipua kwa haraka:-) Nimekwisha atika atika baadhi ya mbegu ndani kwenye makopo kama kawaida:-) ZAIDI MAENDELEO YA BUSTANI YATAKUJA....JIONI NJEMA NDUGU ZANGU!!

12 comments:

Anonymous said...

Hongera kwa kazi nzuri ya kilimo. Sie tunakuja kula na kusubiria bustani itakavyopendeza. Ila umewahi sana mwaka huu?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana ndugu yangu..usiye na jina:-D..kuhusu kula yaani karibuni sana ...nimewahi ndiyo mikono inawasha....

Rachel siwa Isaac said...

Hongera KADALA..Nitakuja kukusaidia mwaka huu.

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI WW...UNASEMAGA TU:'( Jembe linakusubiri hapa...

Rachel siwa Isaac said...

Shaka ondoaaaaa....KADALA..Mwenyewe utashangaaaa!!!!!

Rachel siwa Isaac said...

Shaka ondoaaaaa....KADALA..Mwenyewe utashangaaaa!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Haya KACHIKI shaka imeshatoka Nakusubiri:-D

sam mbogo said...

ulimaji wa namnahii kwangu mimi nashindwa, sisi wakukaya unyamwezini/usukumani hupenda maeneo yaliyo wazi na makubwa,sasa kipengele cha kabstani huwa naona kananitia uvivu,ila wifi yenu na watoto,(mke wangu waubani mamsap roho yangu..) wao hasa ndo kumekucha sasa hivi tayari washa panda mbogamboga.ugomvi unatokea wakisafiri kidogo nakuniacha mimi nyumbani wanakuta mazao yao yako hoi taabani baba hataki kumwagilia maji.anyway hongerakwa kulima,.Rachel mbona wewe hatuoni bustani ya ulanzi? kaka s

Rachel siwa Isaac said...

Sawa KADALA...

Kaka sama huwatendei haki jamani..yaani juhudi ya Wifi na wanangu yoote wewe unawavunja nguvu.

Mimi sikuwa na eneo ndugu yangu na hata sasa ni kadogo sana,Lakini nitajaribu vitu vidogo vidogo...kwani nami naona uvivu nataka SHAMBAAAA niangushe Matuta ya Viazi....Tehetehteh.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! ? Na Rachel aka KACHIKIA HUO NI UVIVU TU...LOL . Hakafu nakubaliaba na Kachiki huwarendri wema kuaacha kumwagilia...

Manka said...

Hata mie nimeanza kutifua tifua bustani yangu leo,kila la heri Dada yangu..natamani ningekuwa jirani unipe mbegu za mchicha lol

Yasinta Ngonyani said...

Manka! safi sana. Bahati mbaya sana yaani ungekusanya za figiri pia maboga...ila kabla kuondoka ungenisaidia kwanza chama chiwuyayi....