Wednesday, April 9, 2014

HIVI HII IMEKAJE HAPA ...EBU SOMA! ETI NI KWELI HII au NDIYO MISEMO TU??

Hii nimetumiwa nimejiuliza mwenyewe kama kweli na jibu lake likabaki ni kuguna tu na mwisho nikaona niweke hapa labda naweza kupata jibu...Msaada jamani hapa!!!
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ukitaka majungu oa Mhaya,
Ukitaka mapenzi ya ujanja ujanja na uwizi wa mfukoni oa Mchaga,
Ukitaka uchawi oa Mfipa,
Ukitaka maneno oa Mzenji,
Ukitaka mapishi oa Mtanga,
Ukitaka mume mwenza oa Mzaramo,
Ukiwa na shamba oa Msukuma,
Ukitaka mapenzi ya kuona aibu oa Mhehe,
Ukitaka kubana matumizi oa Mpare,
Ukitaka kisukari oa Mwarabu mara tende mara halua,
Ukitaka kujichanganya oa Mkerewe au Mjita,
Na kama unataka kuwachanganya mtu na dada yake oa Mrangi,
Ukitaka kubishana oa Mnyirmba
Ukitaka kupigana oa Mkuryaa,
Ukitaka kuzaa sana oa Muha,
Ukitaka kubembelezwa na kudanganywa oa Mnyamwezi
MMMMMHHH! PANA UKWELI HAPA KWELI ...NAONA WANGONI HATUPO KWENYE ORODHA:-)

9 comments:

Anonymous said...

mh! napita tu, sioni ukweli wake lakini.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa kupita na kuacha neno lako la moyoni.

Anonymous said...

Da Yasinta pana ka ukweli fulani hivi! Najiuliza hivi kuna tofauti kati ya wangoni na wahehe? By Salumu.

Nicky Mwangoka said...

Makubwa

Anonymous said...

Ukitaka mapenzi ya kweli oa Mngoni.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu! Kama kuna kaukweli fulani je ni kepi?...tofauti ya wangoni na wahehe ...mmmmhhhh, kwani wangoni nao wana aibu?
Kaka Nicky...yaani madogo yana nafuu.
Usiye na jina wa 10:27 PM ....naoba uneongeza kuhusu MNGONI. Je una uhakika?

NN Mhango said...

Kweli hii imekaa kinomi hasa kwa wale wasiojua mila za kibongo. Ningependa kujua ukitaka nini ndiyo uoe mngoni.
Je ukioa mmasai, mmakonde, mngindo, mnyasa, mnyakyusa, mbena, msafwa, mnyambo, mhangaza na, mkutu, mnyiramba, mnyaturu,muarusha na mbondei unataka nini?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! Kinoma hasa. Mmmhhh kwa vile mimi ni MNGONI sisemi kitu labda kuna aliyeoa MNGONI atasema:-)...Pia ningependa pia kufahamu hayo makabila mengine auloyataja pia...

Nancy Msangi said...

Hahaha nimeipenda sana hii message Da yasinta km hutojali whatsap me 0768810848