Wednesday, December 11, 2013

TUSISOME MAWAZO YA WENGINE!

Ni hatari kwa mtu kudhani kwamba, anajua kila ambacho kinaendelea kwenye mawazo au hisia za mpenzi wake. Kuna uwezekano mkubwa hisia zako zinaweza zisiwe sahihi, kama ambavyo mara nyingi imekuwa ikitokea. Kuna migogoro mingi ambayo chanzo chake ni hisia potofu, hisia zitokanazo na mtu kujaribu kuingia kwenye mawazo au hisia za mwenzake.

Hebu fikiria, umeingia ndani mwako kutoka huko utokako. Unamkuta mumeo/mkeo akiwa amekunja uso. Kabla hujamuuliza chochote unaanza kufikiria kwamba, amekasirika kwa sababu leo umechelewa kurudi nyumbani kwa nusu saa tu. Unaanza kuwaza kwa kulaani kwamba, mumeo/mkeo siyo mtu wa maana kwa sababu ya wivu. Unaweza kufikiria kwamba, usiku huo utamwambia ukweli na kama ni kugombana ni afadhali iwe hivyo, halafu unamuuliza "Vipi mbona uko hivyo, nini tena?"

Mumeo/mkeo anakujibu "Hapana, nina taarifa mbaya, nimesimamishwa kazi kutokana na tuhuma fulani...." Unabaki ukiwa umepanua mdomo, kwa sababu uliingia kwenye mawazo yake na ukawa umekosea sana. Mfano huu ni wa jambo dogo, kuna wakati tunaweza kuingiza mawazoni mwetu fikra kwamba, wenzetu hawatupendi kwa kudhani kwetu kwamba tunaweza kujua yale yanayoenda mawazoni mwao. Kutokana na kufikiri kwetu hivi, tunaweza kuanza kufanya mambo ambayo sasa ndiyo yatapelekea wapenzi wetu kuacha kutupenda.
HABARI HII NIMEITOA KWENYE KITABU CA MAISHA NA MAFANIKIO KILICHOANDIKWA NA MUNGA TEHENAN...JITAMBUE
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hii huwa inatokea mara nyingi sana na watu wengi wamepoteza marafiki zao kwa hili jambo la kusoma mawazo...ni bora kuuliza....

4 comments:

Anonymous said...

Ndio mambo ya kudhani! Jamani nimetoa Hilux mpya "Columbia" nataka nikamchukue Kapulya nikamtembeze! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu:-) ni kweli mambo ya kudhani eti .....Bonge la ujumbe hapo:-) Kapulya

Unknown said...

Mmh nimejifunza kitu hapo da yasinta, ubarikiwe na uendelee kutupa elimu.

sam mbogo said...

Kwa mtazamo wangu,nafikiri siyo vibaya, KUDHANI AU KUMDHANIA MTU. PIA SI VIBAYA KUSOMA MAWAZO YA MTU. inapotokea hivyo katika mambo hayo mawili niliyo sema kwa hakika matokeo yake utakuwa umejifunza kitu,na kama nia yako ni nzuri basi utakuwa huru zaidi na kuwa makini utakapo kutana na mtu anayeonyesha dalili yeyote ambayo wewe kwako yaweza kuwa kikwazo,utajiuliza marambili kablaya kuchukuwa uamuzi. pia waswahili husema USISEMENENO LITAKUKUTA NENO.kaka s