Monday, November 18, 2013

HABARI NJEMA:- NI KWAMBA LEO NIMEPATA UNGA WA MAHINDI:- LEO MLO UGALI NA MBOGAMBOGA:-)!!!

Habari za wikiendi ndugu zanguni...kama mnakumbuka vizuri niliwaambia kuwa niliishiwa unga wa ugali. Sasa katika kutafuta tafuta nimepata kama muonavyo katika picha. Unga ni mweupe kama wa mahindi ya nyumbani. Huu unatoka Venusuela...Haya sasa karibuni kula ugali:-) NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMATATU!!!

5 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta. Huo unga mfuko una kilo ngapi? Na unanunua bei gani? Maana kama Venezuela wanaweza kuuza Sweden, vipi TZ ishindwe! By Salumu.

John Mwaipopo said...

usitukaribishe nguna, tukaribishe ugali

tanexa said...

Asante sana Yasinta kwa kujali made in Tanzania.Changamoto hapa ni jinsi ya kutangaza bidhaa za Tanzania huko ughaibuni.Unga wa nafaka mbalimbali unapatikana na jukumu watanzania kuwashawishi wafanyabishara wa huko ughaibuni jinsi wanavyoweza kunufaika na bidhaa kutoka Tanzaia.Unaposema unaipenda Tanzania lakini huchangii uchumi wake katika kupromoti mazao yake ughaibuni unamaanisha nini????

Yasinta Ngonyani said...

Kaka salumu huo ni mfuko wa kilo moja kwa mahesabu ya haraka haraka inaweza kuwa kama elfu saba vile.....Kaka Mkuu Mwaipopo duh! karibu sana sana yaani nilikumiss kweli wala usiwe na wasiwasi utapata UGALI KAKANGU:-)

Tanexa karibu sana katika kibaraza hiki...Na ahsante kwa mawazo mazuri.

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur