Monday, March 16, 2009

UTARATIBU WA SHULE

Ngoja leo tuangalie kuhusu utaratibu wa shule, nikiwa na maana utaratibu wa shule hapa Sweden na Tanzania. Kwani binafsi nimamaliza shule Tanzania na sasa naishi hapa. Kama si kusei nilipokuwa mdogo nakumbuka hata siku moja sijawahi kuona au kmwona au hata kusikia ya kwamba mzazi anakwenda shuleni kusikia maendeleo ya mtoto wake. Pia sijawahi kuona mzazi anakwenda shuleni siku moja kuwa na mtoto wake. Yaani kuona anafanya nini kweli yupo shuleni?

Hapa niishipo sasa nimeona na pia binafsi ni mzazi. Kwa hiyo kama mzazi nina jukumu kwabwa la kuwalea watoto wangu. Lakini pia ni sheria na pia ni utaratibu kila mzazi anaitwa shuleni kwenda kuona/kusikiliza maendeleo ya mtoto wako. Na hapo sio inaanza shule ya mzingi tu, hapana, ni tangu chekechea. Na sio mzazi/wazazi na mwalimu tu hapana na mtoto mwenyewe anakuwepo. Na jambo hili huwa linafanyika kila muhula mpya unapoanza. Unaambiwa jinsi mwanao alivyo na juhudi aa jinsi alivyo mzembe na kama anahitaji mwongozo gani. Leo nimekuwa shuleni kusikiliza maendeleo ya mtoto wangu ndio maana nimekumbuka kwa nini nilipokuwa nasoma mimi au mbona wazazi wangu walikuwa hawaji kusikiliza maendeleo yangu. Halafu nimekumbuka kumbe hakuna utaratibu kama huu.

3 comments:

Christian Bwaya said...

Nchini bongo, mtoto atajijua mwenyewe. Akipenda kuishia mtaani na 'shughuli' zake, hewalaa. Almuradi tu awe makini muda wanaotoka wenzie shule nae awahi home na uniform.

Halafu wazazi bwana. Dogo akifeli lamama zote kwake! '...toto lenyewe hutaki kusoma..'

shule yenyewe ya Kata, haijamaliziwa kujengwa halafu walimu wa voda fasta wanachojua ni kusaka urafiki na wanafunzi 'wenzao'. Unategemea nini?

Anonymous said...

sio kweli,Bwaya hata bongo siku hizi mambo ni tofauti kuna shule pia mzazi unakwenda kuzungumza na mwalimu wa mwanao, lakini ni hizi shule za private binafsi huwa nakwenda kila term unatakiwa kwenda mara moja.

Kwa shule za serikali hizo nazani bado sina uhakika,kuna nyingine ni nzuri na zinamfumo mzuri.

Mzee wa Changamoto said...

Utaratibu wa kuwaweka wazazi karibu na maendeleo (na hata maanguko) ya watoto wao ni mzuri saana. Nashukuru kuwa wazazi wangu walikuwa wakipitia madaftari yangu kila siku. Nilikuwa na sehemu maalum ya kuweka mfuko wangu wa daftari na walikuwa wakipitia kila usiku hata ninapokuwa nimelala (maana nilikuwa nalala mapema kwani kulikuwa na mwendo saana toka Lutheran Junior Seminary mpaka Kigurunyembe) na tulikuwa tukiondoka mapema. Kwa hiyo maendeleo yangu yalijulikana kila siku. Wangejua nimepata vipi, nimekosea wapi, nina tatizo gani na hata kama ningechana karatasi kwenye daftari wangejua. Kwa ujumla ilinifanya niwe "organized" katika kazi zangu daftarini
Sitadanganya kuwa pale nilipoanza kuishi mbali nao nilirudi nyuma kiasi maana sikuwa na pressure ya kunifanya nijitahidi na kumbuka kuwa wakati huo akili nayo si njema kuamua. Ni kuendeshwa na hulka na wenzako.
Lakini utaratibu huu ni mzuri na nashukuru kama kuna wanaoufuata.
Ila nadhani ni wakati wetu kuamka. Kutosubiri kuitwa mara moja kwa muhula. Kama tutakuwa tukifuatilia maendeleo yao kila siku sidhani kama kutakuwa na tofauti na wale wanaojumuika kila term / semester.
Baraka kwako Dada