Tuesday, March 10, 2009

MAVAZI YETU /MAISHA YETU

Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi juu ya mavazi yetu. Ni vazi gani ni la mwanamke na lipi ni la mwanaum? Pia siku hizi ni aibu tupu, utakuta mama na heshima yake anavaa nguo za mtoto wa miaka 10. Blauzi fupi kiasi kwamba tupo linaonekana na pia suruali ambayo inabana makalio (matako) na penginne hata nguo ya ndani (chupi) kuonekana. Wewe kama unajua ni mnene kwanini usishone/nunue nguo za saizi yako?

Hali hii haiko Ughaibuni tu, kwani sasa hadi kwetu Afrika imeshaigwa. Watu wanaacha mavazi yao mazuri ya asili, ya heshima pia utamaduni. Inasikitisha sana kuona utamaduni wetu(wa kiafrika ) unapotea. Labda pengine wengi wanafikiri vitu/nguo vitokavyo Ughaibuni ni BORA zaidi. Binafsi napenda sana utamaduni wetu na mavazi yetu. Sijui wenzangu mna mawazo tofauti nami? au?

14 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

MIMI SIJUI KABISA KWANI HISTTORIA INAONYESHA KABLA YA KUJA KWA WAKRISTO, WAAFRIKA WALITEMBEA UCHI AU WALIFUNIKA TU MBELE KWENYE SOMETHING NA KWNGINE KUKABAKIA TUPU. LABDA WAAFRIKA WANARUDIA UTAMADUNI WAO

Albert Kissima said...

Nakubaliana nawe dada Yasinta,uvaaji wa akina dada wengi hata na wamama umekuwa ni wa hovyo kabisa.Tunalazimika kuushuhudia utamaduni ambao hatukuuzoea.Kweli ,kuna tamaduni nyingine tunazipokea, lakini zinakuwa ni za kimaendeleo zaidi, yani za maendeleo chanya.
Wengi haturidhishwi na uvaaji huu wa nguo, sasa solution yake ni nini?
Nafikiria solution, then nitarudi tena.

Albert Kissima said...

Watoto wadogo wa leo wanatakiwa wakuzwe ktk maadili mazuri,yani wakue wakiwa wanatambua lipi baya na lipi zuri.Wazazi wanatakiwa wawe makini ktk makuzi ya watoto kwani mazingira yanachangia sana ktk tabia ya mtoto.Kama mtoto amekulia ktk mazingira ambayo mzazi na ndugu zake wanavaa kiajabu ajabu,au familia ambazo matusi yamekua ni kiunganishi ktk maongezi,ni dhahiri kuwa mtoto ktk mazingira haya atanakulia utamaduni mbaya na ni wazi kuwa ataendelea kuutumia hata atakapoanza kujitawala.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa inategemea na malezi katika familia/walezi. Lakini pia dunia ya leo watu wengi hupenda sana kuiga hii ndio inaharibu utamaduni. Nafurahi sana tuwapo TZ binti yangu anapenda sana utamaduni wetu.Nategemea ataendelea hivyo.

Anonymous said...

Yasinta hao watu hawavunji maadili ila wanarudia utamaduni wao wa miaka mingi kabla wazungu hawajaja.Mavazi unayosema yanaendana na utamaduni wetu,ukiangalia kwa undani utaona kuwa mengi yaliletwa na wageni.Mfano halisi wa mavazi yetu ya asili ni kama yale wanayovaa wahadzabe wa Arusha.
Kama unaona hizo sketi wazovaa siku hizi ni fupi unalionaje suala la mavazi ya Wahadzabe na mbilikimo wa misitu ya Congo?

Simon Kitururu said...

Mimi na uhakika na ya jinsi yakuwa uchi.

Ya mavazi niko shule najifunza.

Yasinta Ngonyani said...

Katawa, Lakini kwa nini tusifuate mavazi ya utamaduni wetu yenye heshina na kufuata yanayoletwa na wageni ambayo nusu ni kutembea uchi?

Simon Ni kweli afadhali kutembea uchi kabisa kulikoni. Yaani basi tu

Anonymous said...

Yasinta nashukuru kwa kukubaliani nami kuwa tufuate mavazi yetu ya asili.Kwa hiyo tuanze kuvaa kama Wahadzabe.

Yasinta Ngonyani said...

Ndio nakubaliana nawe kwa kuwa sipendi utaduni wetu upote. kwa hiyo nipo nawe tuanze kuvaa wahadzabe. Kwani ni ukweli ukiwa huku niliko ukivaa nguo zetu watu wanapenda sana na wanaulizia we wa wapi?

Albert Kissima said...

Katawa kwani wewe umekulia kwenye utamaduni wa watu wanaovaa ngozi,magome ya miti au kujifunga majani? Ingekuwa ndivyo basi sasa hivi ungekuwa unajifunga majani,au kujisitiri na ngozi. Ndio maana hata mtoto wa kihadzabe hata akiziona nguo hawezi kuibuka tu na kuanza kuililia nguo ili aivae,kwa nini?kwa sababu si utamaduni wake.
Sisi hatujaukuta utamaduni wa kutembea uchi, utamaduni tulioukuta ni wa kuvaa nguo zinazositiri miili yetu kwa uzuri kabisa yani nguo za heshima.

Ninachomaanisha hapa ni kwamba tamaduni za mababu zetu ambazo sisi hatujazikuta na hatujazitumia inabidi zibaki kama historia na usizichukulie kama ndio tamaduni zetu.
"Nachelea kusema kwamba taratibu na kanuni alizokulia mtu ndio utamaduni wake" aliyoyaishi babu yangu kama mimi sijayaishi,utamaduni huo wa babu yangu hauwezi kuwa wakwangu.

Jamani, nahitaji kujifunza zaidi,msichoke kunielewesha,ni mawazo yangu tu. Amani iwe nanyi.

Anonymous said...

Kisima,kwa maelezo yako umeonyesha kuwa utamaduni unabadilika.Kama utamaduni unabadilika kuna tatizo gani kwa hawa wavaaji wa nguo ndefu kubadilika na kuanza kuvaa nguo fupi?.Kizazi kijacho kitarithi utamaduni huo kama Yasinta alivyorithi kwa bibi zake.Kumbuka kizazi hiki nacho kitakuja kuitwa cha babu na bibi.

Albert Kissima said...

Nakubaliana nawe Fred,utamaduni unabadilika,lakini lazima tuangalie unabadilika kivipi,
Leo hii ukimwona mtu anatembea uchi barabarani ni lazima utashangaa,na ni lazima utakemea hali hiyo.
Wabarbaigi mpaka leo wanajifunga ngozi au majani ya miti,wao wanaishi hivyo kwa sababu hawajaruhusu tamaduni za kutoka sehemu ningine.
Fred, huoni na sisi tunaweza kusimama kidete na ku umaintain utamaduni wetu mzuri na hatimaye ukaigwa vizazi hata vizazi?
Mababu zetu wangeweza ulinda vizuri tamaduni za enzi hizo ,ungekuta mpaka leo tunaziishi.

Anonymous said...

Kissima,kwa sasa nikiona mtu anatembea uchi siwezi kshangaa wala kukemea bali nitaheshimu maamuzi ya huyo mtu kwa kuwa anafanya jambo alipendalo.

Albert Kissima said...

Fred, kwahiyo hata walarushwa,mafisadi,wanaowaua maalbino n.k tuwaache tu kwa sababu wanafanya wayapendayo?