Thursday, March 5, 2009

SALAAM KUTOTKA SONGEA

Sikuweza kuacha kuchukua picha hii je? kweli tunafanya hivyo?

7 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nani aache? wewe unajua utamu wa chungwa? walioandika kibao hiki wanabishana na mungu aliyesema tufanye mpaka cheee?

agha mi siacha, na ukimwi sipati.
cjui yasinta umeacha?bibu

Christian Bwaya said...

Kuwaambia ni rahisi. Kufanya unachowaambia hapo ndiko iliko kazi!

Tatizo la UKIMWI kwa maoni yangu, naona si taarifa maana tunazo. Na zimekuwapo juhudi kubwa za kusambaza taarifa (hata kama zingine zaweza kuwa si sahihi sana.

UKIMWI umebeba hata wasambaza taarifa (huenda hata mwandika bango hili naye ndio hivo tena).

Tatizo la msingi ni namna gani tunaweza kuzitumia taarifa hizo kukabiliana na janga lenyewe kwa ufanisi.

Vinginevyo, tunaweza kujikuta badala ya kuelimisha tunakuta tunazalisha tatizo lingine ambalo halikuwepo.

Naacha (kama anavyosemaga Mkodo)

PASSION4FASHION.TZ said...

Hahahaha,Kamala umenichekesha sana,mmmh! we haya we Lemi aliimba jamani gonjwa hili limekaa pabaya kwenye kifundo cha muwa,akaambiwa kakosa adabu mwimbo ukapigwa marufu

Msanii mwingine yeye aliimba kwa lugha ya kisukuma,akasema ukimwi ungekuwa unapatikana kwenye chai basi yeye angeacha kuinywa,

kama ni kwenye maji nayo angeacha kuyanywa, kaimbi kila kitu kama ni chakula angeacha lakini hapo je?mmm pagumu kuacha hata yeye kashindwa hapo hawezi kuacha.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe mapadre wanashindwa kuacha japo ni katika jina la yesu, iweje wewe?

Anonymous said...

Watu wanashindwa kuacha sigara hata kama akiambiwa kwamba mapafu yake yameshajaa moshi na asipoacha atakufa. Sembuse hapo...Na hii inazua mjadala mwingine. Kwani maisha ni nini hasa? Wakati mwingine ukifuata masharti yote ya hawa "wataalamu" basi hutaweza kuishi kwani karibu kila kitu utaambiwa ni kibaya na kina madhara. Nimeshaambiwa mara nyingi sana kwamba niache kula ugali kwani ugali ni carbohydrates na hizi zinanenepesha na unene una madhara mengi mno kwa afya. Sasa mimi nikajiuliza, Msukuma kweli tena Mnyantuzu wa Bariadi kweli niache kula ugali? Kweli? Nadhani nimeshakisema ninachotaka kukisema japo pengine sijakisema!

Anonymous said...

Wakona KuSongea?
Usisahau mdojolela, ngowani, na matangamanga kwa afya yako. Kakako

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nanyi kuambiwa kuacha kitu ukipendacho si rahisi. Na pia ni kweli siku hizi kila kitu tunaambiwa usifanya hivi ni hatari kazi kwelikweli.

Kakangu hapo usiye na jina nene niwuyili ngowani,mdojolela, matangamanga na malembi nilili kweli