Wednesday, August 21, 2013

BINADAMU NA MAZINGIRA:- KUFANYA UAMUZI NI MUHIMU KATIKA MAISHA

Nimeamka na kama kawaida nikiwa na mawazo mengi kichwani, mmmhhh nikaona ngoja niende kukimbia ili kuweza kufanya takafari. Unajua unapokimbia au tembea mstuni unaweza kuchanganua mawazo vizuri sana maana kupo tulivu. Basi nikaanza kuaendelea kuwaza hili ambalo ni muda sasa nilikuwa nikiliwaza.:- Linahusu jinsi ilivyo muhimu kufanya uamuzi...Hivi ndivyo nilivyowaza:-
Nikaanza hivi, Maish huenda bila kuamua? na nikajipa jibu mmmh:- Maishahayaendi hivyo na hata siku moja haijatokea mtu asiyejue anataka nini maishani kufanikiwa au kutulia. Kama mtu ameamua kufanya biashara  kwa mfano ya genge basi inabidi ajizatiti sana na biashara hiyo na aipange mipango yote ya kuikuza.
Na nikajiuliza je kama mtu anataka kusoma afanyeje? Kama mtu ameamua kusoma masomo fulani au kufanya kazi aina fulani, basi inabidi azingatie hilo na wala asiyumbe.
Kila siku huwa tunasikia watu wakisema , "yule jamaa alianza kuuza chapati na vitumbua tu, lakini angalia sasa alivyotajirika ana mabasi na maduka mji mzima". Au mfano mwingine utasikia wakisema "yule jamaa alianza masomo yake kwa njia ya posta tu lakini sasa yupo chuo kikuu". Hizi kauli huwa zinatamkwa sana lakini bila shaka  hatujawahi kujiuliza inakuwaje hadi mtu kama huyu kufikia juu kiasi hicho kutoka alipoanzia ambako wengi wanadhalau na kukata tamaa?
Kwa hiyo hapa nikagundua kwamba:- Tukianza kujiuliza sasa tutajua kwamba sababu kubwa ni mpango inayotokana na kujua kwamba anataka kitu gani maishani mwao. Kwa sababu wanajua wanakokwenda wanachokitafuta, hata mambo yakienda kombo watangángánia tu kufanya shughuli zao. Wale wasiojua wakiyumba kidogo tu huacha kile wakifanyacho na kukimbilia kingine.
UJUMBE:- Ninachotaka kusema hapa katika maisha mtu unatakiwa kuwa  malengo hata kama malengo hayo utafanikiwa baada ya miaka kumi. Kwa kuwa ni malengo ndiyo ambapo utaweza kwanza kutulia na baadaye kufika kule unakokutaka
KAMA HUJAWEKA MALENGO KWA UNAYOTAKA KUYAFANYA KATIKA MAISHA FANYA SASA.
NAWATAKIENI KILA LA KHERI NA TUSIWE NA TABIA YA KUKATA TAMAA: KAPULYA

3 comments:

ray njau said...

Hakika hiyo ndiyo siri ya maisha na mafanikio.Asante sana mwalimu Yasinta kwa darasa la leo.

Salehe Msanda said...

Habari
Ni kweli bila malengo hautajua wapi unakwenda na wapi umefikia.
Wengi wetu tunakabiliwa na ugonjwa wa kutofanya maamuzi na kutenda kwa kisingizio kuwa nimechelewa ukiluliza umechelewa kutoka wapi
Jibu hakuna. Tunatakiwa kujikagua na kufanya maamuzi na kutenda tukiweka na subira katika kle tulichoomua kufanya na kutenda.
Kila la kheri.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! karibu sana hapa tunakumbushana kwa vile kila mtu anajua msingi wa maisha ni nini ila kitu kigumu ni kutozingatia.

Kaka Salehe! Ni kweli ulichosema wengi tunafikiri tumechelewa na pia haiwezekani tunasahau ya kwamba hakuna kisichowezekana katika maisha ili mradi ukijizatiti tu.