Tuesday, October 10, 2017

HAYA MATUNDA NI MATAMU SANA....YANAITWA MAPERA

 Mapera yakiwa mtini na hapo unaweza kujua lipi lipo tayari kuliwa.... kuna wengi wanashindwa kula mapera kutokana na kuwa na .....
....mbegumbegu kama uonavyo hapa...basi ni bora kunywa juisi  yake ni tamu sana....Nimeyatamani sana mapera leo....Je kuna tunda wewe umelitamani kwa hivi karibuni?

7 comments:

NN Mhango said...

Umenikumbusha shule ya msingi tukiyala sana haya madude utadhani ndege.
Ama kweli ya kale dhahabu. Hapa Kanada sijawahi kuyaona japo tuna matunda mengi na mboga kama vile nyanya chungu na mlenda aka bamia.

Yasinta Ngonyani said...

Nimecheka mpaka tumbo laniuma. Eti kama ndege...itabidi nije huko kuzifyata nyanya chubgu ili nikuletee na mapera ila ya kopo:-)

NN Mhango said...

Mapera ya kopo si mapera. Ninaposema nyanya chungu huku naaminsha orijino siyo kopi kama hayo mapera ya makopo.

Yasinta Ngonyani said...

Nilikuelewa kaka lakini kama hakuna orginal basi hata kopi yafaa au wasema vipi? au subiri nitakuchukulia toka Ruhuwiko...

NN Mhango said...

Inshallah na shukrani sana.

Juma Mtwana said...

Nimeyamisi sana sijayatia mdomoni siku nyingi sana

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu Mtwana fanya kama kaka Mhango karibuni Ruhuwiko mtakula tani yenu au nawe unataka nikuletee...?