Mwanamke Mwenyeumri wa miaka zaidi ya 120 mkazi wa Peramiho B wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye huenda akawa mmoja wa wa watu wenye umri mkubwa duniani Bi. Sophia Haule ambaye alishuhudia vita ya kwanza ya dunia ,ya pili na vita vya maji maji anaiasa jamii kutoshabikia vita.
Ni simulizi ya kusisimua ya bibi. Sophia haule mwenye umri wa miaka 120 ambaye alishuhudia vita ya kwanza ya dunia mwaka 1914-1918, vita ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi mwaka 1945 na vita vya maji maji na kuona machungu ya vita na anasema vita si vya kuvikimbilia.
Varelia ngonyani ni mwenye miaka 77 ni mtoto wa bibi sophia haule pamoja na kueleza changamoto za kumtunza mzee huyo menye umri mkubwa zaidi lakini anaeleza mambo aliyosimuliwa na mama yake yaliyokuwa yakifanywa na machifu likiwemo la kuzikwa na binadamu akiwa hai pindi chifu anapozikwa.
Jimbo la Peramiho limebarikiwa kuwa na watu walioishi umri mkubwa wa miaka 90 hadi 100 ambapo mwenyekiti wa kijiji cha peramiho b anasema anajivunia jambo hilo.
CHANZO: ITV
2 comments:
Hebu weka vizuri picha ya kigoli huyu lau tupate vitu vyake sawa sawa.
Hii ni rekodi kwa kweli.
Post a Comment