Thursday, November 23, 2017

NDUGU ZANGU:- TUTAFARI KWA PAMOJA MALEZI YA WATOTO WETU

 

Ukimkosoa sana mtoto na kumkaripia mara nyingi unampunguzia ujasiri na uwezo wa kujitegemea awapo mtu mzima.
Msaidie kwa upole, muelekeze, mtie moyo, akikosea mweleze jinsi Mungu anavyoumia kwa kosa alilolitenda.
Usimwambie kuwa hana jema hata moja hasa akiwa binti, maana siku moja kuna vijana wataona jema lake na watamwambia kisha ataweka USIKIVU Wake kwao.
Muombee mwanao/wanao, Mfundishe/wafundishe kuomba mwenyewe/wenyewe  Bwana atamsaidia/wasaidia.
Hii ni pamoja kumchapa mtoto viboko, ni kumwongezea usugu tu 

4 comments:

NN Mhango said...

Hiyo si kweli vinginevyo awe mtoto wa kizungu au aliyezaliwa bila kujiamini. Sijui wengine wanasemaje. Hapa lazima tujitahidi kutofautisha mila na desturi za wahusika. Ni bahati mbaya kuwa waafrika tumekuwa tukitumia mifano na majaribio yaliyofanyika ulaya bila kuangalia utamaduni na mazingira yetu yanasema na kutakaje. Siwezi kuongea mengi hapa. Ila kwa uzoefu wa malezi yangu sioni kama dhana hii ni kweli.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka M...Naweza kukubaliana nawe kwa asilimia fulani ...Ni kwamba tunapoteza sana utamaduni wetu, mila na desturi hususani hili ...lakini je mbinu ipi ni bora?

NN Mhango said...

Mbinu bora ni ile iliyokulea wewe nami tukawa tulio sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nawe asilimia 100%