Friday, February 27, 2009

USAFIRI TANZANIA/DAR ES SALAAM

Muda mrefu imekuwa inasemekana kutakuwa na mabadiliko ya usafiri nchini Tanzania. Lakini mpaka leo hakuna kinachoonekana. Nina maana kwa sasa hasa jijini Dar es salaam kuna tatizo kubwa la usafiri yaani daladala ni nyingi mno kiasi kwamba ni fujo tu. Afadhali kutembea au kutumia baiskeli kwa jinsi foleni za daladala zinavyosongamana. Naweza nikasema hakuna maana kuwa na gari Dar, kwenda kazini inabidi ujihimu mapema sana na ukichelewa basi itakuwa ule mtindo wa foleni. Na ukitaka kwenda sehemu ni afadhali ujue ni muda gani mzuri sio kuondoka tu.

Sijui mwenzangu mnasemaje? Kwani binafsi ningependa au pendekeza daladala zote zitolewe na kuwe na mabasi makubwa na pia train ya haraka. Nadhani kungekuwa na nafuu sana kwa wananchi. Kwa sasa naweza nikasema kwa kweli ni fujo, fujo, fujo sana. Maana magari mengi sana, pikipiki nyingi mno na daladala ndo uchafu tu.

4 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Ndiyo maana nilipokuwa nakwambia sipandi gari pale tulipokuwepo ulidhani natania? Nilikwambia najua toka hapa(tulipokuwepo) kwenda upande ule wa kushoto ingekuwa kazi hadi kufika kituo nilichokihitaji. lakini nikasema ukipanda kwenda upande ule wa kulia poa sana. UKACHEKA SANA nadhani umeona baomgo yetu izoee tu. Nilicheka sana uliposema tumepita huku tukaambiwa zungukeni huku. DUH! ilikuwa kazi kweli.

Mara eeeeh Markus Tupo Mwananyamala baada ya dakika chache tutakuwa geto!!
Moyopni nikajua ngoja upambane na usafiri halafu usimulie kwanza. DUH! kama niliota ukasema aise hii kali DAR ni noma.
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha POLE SANA JAMANI nawamiss sana woteeeee mwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

PASSION4FASHION.TZ said...

Hiyo ndio bongo dada,umejionea mwenyewe mambo mdundo kama wenyewe wasemavyo.

Ustarabu bado sana hasa kwenye daladala dada bora utembee kwa mingu kama ni mwendo ambao unaweza kutembea.

Ila mtani wangu unablog nzuri sana na wewe nimeipenda nimeijua hivi karibuni tu ukiwa likizo.Karibu sana wa kunyumba.

Mzee wa Changamoto said...

Ndio kwetu huko Dada. Nasio aliimba kuwa "don't worry about the pretty things you hear they say". Ndio haohao. Kwenye hotuba ukiwasikia unaweza kufungasha kila kilicho chako kurejea nyumbani. Ukifika home unajiuliza kama walikuwa wanasema wanalojua ama ndio Da Subi anayosema kuwa "siasa si hasa, ni visa na mikasa." Afadhali umeona maana hata Lucky Dube alisema "till you get there, you see for yourself". Sasa siku nyingine ukiwa unawasikia wanatoa hotuba fanya alichosema Dennis Brown kuwa "sitting and watching fool by themselves when they should always thinking of getting to know themselves".
Pole Da Yasinta na karibu katika ULIMWENGU HALISI wa Bongo yetu

Yasinta Ngonyani said...

Markus nimekusikia:)

passion4fashion.tz karibu sana.

mzee wa changamoto umsema kweli kabisa.