Tuesday, October 9, 2012

HII ITAKUWA PICHA YA MWAKA KWA KWELI ..!!!!

Inasemekana maziwa ni lishe bora kwa watu/hasa watoto lakini ndiyo hivi kweli? Salama hapa?
Ngoja nisikilia hizi chuchu nyingine ili wengine wasije wakachukua....Nimewahi kusikia kuwa ni hatari kunywa maziwa bila kuchemsha  yaani moja kwa moja kama mtoto huyu. Je ni kwa binadamu tu au?Maana Ndama hadhuriki..Kaaaazi kwelikweli hapa..sijui mama alikuwa wapi?

8 comments:

Ester Ulaya said...

hii kweli ni picha ya mwaka nimeipenda hii.....kweli kunywa bila kuchemsha ujue binadamu tuko delicate sana ni hatari ndo maana twashauriwa yachemshwe..........

Ester Ulaya said...

hii kweli ni picha ya mwaka nimeipenda hii.....kweli kunywa bila kuchemsha ujue binadamu tuko delicate sana ni hatari ndo maana twashauriwa yachemshwe..........

emu-three said...

Hapana hii sio salama na ni hatari, hebu fikiria huyu mnyama akiamua kupiga teke, si anaweza akampofa huyu mtoto! Sijui ni kichekesho au ni kweli, maana mambo ya mtandao yana miujiza yake

Mfalme Mrope said...

Ni kweli kaka Emu-three.. hii si salama hata kidogo. Kuna uwezekano wa kuambukizwa na vijidudu vya magonjwa kama vile E-coli na pia huyo mnyama akipiga teke ni hatari tupu...

Emmanuel Mhagama said...

Nakubaliana na wadau kuwa ni hatari. Lakini pia mtakubaliana na mimi kwamba 'reaction' ya mwili inategemeana sana na mazingira anayoishi mtu. Kwa habari ya kupigwa teke hapo nakubali kwamba ikitokea hiyo maisha ya huyu dogo yapo matatani. Lakini kwa habari ya magonjwa, kama hii ndo style yao ya maisha inawezekana kabisa kuwa hivyo ndivyo watoto wote wa jamii hiyo wanavyokua. Jaribu kufikiri huyu mtoto kapata wapi ujasiri wa kufanya hivyo. Halafu ukiangalia hiyo picha ya juu unaweza kuona kuna mtu mzima anamsadia namna ya kupata hii lishe vizuri. Hata hivyo, kitaalamu inadaiwa moja ya magonjwa anayoweza kupata mtu kwa kunywa maziwa yasiyochemshwa ni TB. Hivyo kama hakuna sababu za msingi za kufyonza direct namna hiyo, basi ni bora kuchemsha. KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

ray njau said...

Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng'avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake hudhoofisha macho na hata kuleta upofu, ngozi kusinyaa na kuonekana iliyozeeka hata kama ni ya kijana.
Vitamini D husaidia mwili kuweza kufyonza madini ya kalsiamu. Bila kuwepo vitamni D kalsium hupotea bure kwa kutolewa nje kama kitu kichohitajika. Japokuwa vitamini D tunaweza kuipata kwenye jua la asubuhi, watu wengi hawawezi kulipata jua hilo. Labda kwa kuishi magorofani au chini ya milima au kutoweza kutoka nje nyakati za asubuhi. Hivyo ni bora kujiwekea uhakika wa kupata vitamini D kwa kunywa maziwa.
Umuhimu wa madini ya Calcium ni kiungo muhimu katika ujengaji wa mifupa. Hasa kwa wajawazito na watoto ambao mifupa yao bado inajengeka. Mwili imara hubebwa na mifupa imara. Na mifupa imara inajengwa na madini ya Kalsium. Ni bora kujijengea mifupa imara, meno na sehemu ya mifupa. Hakika kila mtu anahitaji meno bora na imara, vile vile kalsium hutumika katika misuli (muscle) wakati wa kujikunja na kunyooka. Pia husaidia katika mtandao wa ufahamu mwilini (nerve conduction). Kwa ufupi hayo ni manufaa ya kunywa maziwa, samaki na kadhalika. Mbali na Kalsium maziwa hutupatia madini ya salfa, sodium na phosphoras ambayo mwili pia huhitaji kwa kazi zake mbalimbali.
Maziwa pia hutupatia protini kwa ujengaji wa miili yetu. Mathalan mtoto mdogo wa siku moja huongeza ukubwa na uzito kwa kunywa au kunyonya maziwa tu. Japokuwa kiwango cha protini hutofautiana kulingana na mnyama, pia maziwa ya ng'ombe yana protini ya kutosha. Hali kadhalika katika maziwa ya mbuzi na kadhalika.
Maziwa pia hutupatia sukari (wanga) japo kwa kiasi kidogo lakini kidogo chafaa kuliko kukosa. Na ndio maana japo kwa kunywa maziwa waweza kuhisi nguvu iwapo ulikuwa na njaa.
Nyakati za baridi, maziwa hutumika kama kinywaji moto. Yenyewe peke yake kwenye chai, kahawa au tangawizi. Na wakati wa joto, maziwa hutumika kama kipozeo na kiburudisho tosha. Na kwa nyakati hizi, kila sehemu inaweza kupatikana na maziwa. Kwa asiyependa tunamshauri aanze kuyapenda na kuyatumia.
Maziwa pia hutumika kama dawa kwa kuchanganywa na vitu mbalimbali. Mathalani maziwa ya mama yakamuliwapo kwenye jicho linalowasha, uchafu hotoka na kujihisi salama.
-----------------------------------
**Vigezo na masharti katika usafi na usalama kuzingatiwa!!
----------------------------------

Kiu ya Haki said...

Hii picha inanikumbusha miaka ya tisini wakati tukichunga ng'ombe kulikuwa na dogo m1 alikuwa akinyonya ng'ombe

Anonymous said...

mimi nilitaka kumnyonya ngombe hilo teke lake nililopigwa mpaka leo ninalikumbuka nikimwona huyo dogo hapo mwili unanisisimua na huyo ngombe ni muungwana sana au kwavile huyo anayemnyonya bado mdogo