Monday, November 16, 2015

POMBE SI MAJI....NA WALA SI RAFIKI ILA POMBE NI HATARI KATIKA MAISHA YETU.....


Karibu wiki  mbili  zilizopita nilishuhudia kisa hiki cha kusikitisha ambacho sitakisahau katika maisha yangu. Na kimekuwa fundisho katika maisha yangu. Ilikuwa siku ya  jumatano ya tarehe 5/11/2015, majira ya saa mbili asubuhi. Kulikuwa na mkusanyiko wa wafanyakazi ambao walitakiwa kuwa kwenye mafunzo (kozi). Sasa kwa bahati naweza nikasema bahati  mbaya dada mmoja jina nalihifadhi ila tumwite Maria. Alitoweka ghafla pamoja na bosi bila "wengine" kujua nini kimemkumba  dada Maria.

Lakini baada ya muda habari zikaja ya kwamba kuna wafanyakazi wenzake walipokuwa wakiongea na  Maria , wao waligundua harufu ya kinywa cha Maria ilikuwa inanuka pombe. Nao hawakuishia hapo, wakapeleka ripoti kwa bosi. Na hicho ndicho kilikuwa kisa cha Maria kutoweka ghafla. Kilichoendelea, Maria alipelekwa sehemu ili kuhakikisha kama kweli alikuwa na pombe katika mwili/damu yake. Majibu yalionyesha ni kweli Maria alikuwa na pombe mwilini. Siku ya Maria ilikuwa ni kitendawili alirudishwa nyumbani hakuweza/hakuruhusiwa kuhudhuria ile kozi  siku ile. Na mbaya zaidi ile siku ilipotea bila kulipwa alikatwa mshahara wake.

Niliwaza sana na kumfikiria dada Maria na nikaishia kusema ama kweli sheria kama hizi zingekuwepo dunia nzima :- Basi maendeleo yangekuwepo. Nikawaza  nchi nyingi zingekuwa na maendeleo sana kama zingefuata sheria zilizowekwa. Nikaanza kukumbuka nilipokuwa msichana mdogo nilivyokuwa nikiwaona baadhi ya walimu walikuwa wakienda kupata kupata "chai ulanzi" badala ya chai ile saa nne.  Je? hao vinywa vyao vilikuwa vikitoa harufu kiasi gani? Lakini hakuna sheria yoyote ilichukuliwa  na kama ingekuwa ikichukuliwa sheria je? Wangapi wangepoteza kazi zao?

NENO LA LEO:- NDUGU ZANGUNI POMBE SI MAJI NA WALA HAZITATUI MATATIZO. ISIPOKUWA ZINAHARIBU AFYA NA MWISHO ZINAUA.

No comments: