Saturday, March 8, 2008

8/3 jumamosi Hali ya hewa

Hali ya hewa hapa sweden kwa kweli mara nyingine unaweza kushinda ndani tangia asubuhi mpaka jioni bila kutoka nje kwani ni baridi mmno. Ni mabadiliko makubwa sana kwa mtu atokaye kwetu afrika. Ukiangalia kwetu afrika tunavaa nguo nyepesi yaani sio nzito na sio viatu vikubwa. Mtu unaweza kuvaa ndala na unaendelea na safari. Lakini huku ndugu zangu ni ngumu sana kuvaa hivyo:, unahitaji nguo, koti kubwa, suruali pia viatu nk. Joto/jua tunaliona kuanzia mwezi huu wa tatu, mwezi huu tunaliona jua kwa muda wa masaa tu, tutaendelea hivi mpaka mwezi wa tano sita hapo ndo tutaliona jua. Na pia kutakuwa na joto kidogo kama umewahi kufika Makambako au Njombe ni sawa kabisa miezi hii mitatu. Kwa hiyo mara nyingine unaweza ukakaa na kutamani nyumbani. Nikikumbuka kuvaa gauni na kuvaa viatu au ndala bila soksi natamani sana nyumbani. Nyumbani ni nyumbani hata kukiwa porini au mnasemaje?

Na;Yasinta Ngonyani at 16.42

Toa maoni yako

2 comments:

Anonymous said...

Dadangu pole ndiyo maisha hayo.Lakini unanikumbusha mambo mengi sana ikiwamo jinsi unavyokumbuka nyumbani najua unatamani sana kuwapo huku.Unanikumbusha miji hii makambako na njombe lakini umesahai mbeya yaani nayakati hizi ni ukungu mtupu.Hta pale songea januari panakuwa na baridilakini siyo kama hiyo ya hapo Sweden.Nimefurahi sana kusoma blog hii.Ruhuwiko daima

Anonymous said...

Naam ni tamu sana kusoma blogu ya mahusiano ya kijamii n.k kwani unaipa kile ambacho sijawahi kukusiakia au kuona endelea kutoa mambo ya huko.