Wednesday, February 22, 2012

NI NINI KINAFANYA MAISHA YAWE NA FURAHA?

NI JUMATANO NA NI KILE KIPENGELE CHA MARUDIO MBALIMBALI LEO NI MARUDIO YA November 25, 2008 NDANI YA MAISHA NA MAFANIKIO.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha ya yako/yangu kuwa na furaha kama hatutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yetu. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je? ume/tumesha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo haya.

Mpenzi msomaji katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tulio wengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi muhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha thamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tulio wengi tumekuwa tukililia au kujionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuolewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.

Kuna misemo isemayo kwamba:- mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamume anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mume; poleni sana wanawake tumepotea, badili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.

Na kwa upande mwingine, Mwanamume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegemea kuwa hatabadilika; Mungu ndiye ajuaye kuwa mwanadamu ni kigeugeu, sasa atutendee nini ndipo tulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwa sababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha ni magumu ndani ya ndoa, na wengine umaskini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.

Swali linakuja je? unafikiri kukamatana ugoni na kuonyeshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatua matatizo katika jamii kama watu hawatatumia njia ya kuiweka wazi mioyo yao kwa kile wanachokipenda na kukitamani?

Ni changamoto kwamba kweli tulichokiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli humpendi mwenzako sema tangu mwanzo liwe wazi tusitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ana nafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.

Maisha ya ndoa ni kuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida, kwa furaha na amani bila majuto.

2 comments:

sam mbogo said...

kwa uzoefu wangu,na maishayangu yakawaida,furaha sikuzote ni wewe mwenyewe unavyo amua kuwa. pamoja na uhusiano wowote utakao kuwa nao nii wewe bado ndo ufumbuzi wa furaha yako.katika ndoa furaha ya pamoja ipo hasa kama wana ndoa na wazazi. maranyingi migongano yaweza kutokea na kumnyima mmojawenu furaha. la muhimu hapa ni wote kwa pamoja kuwa makini na migongano ndani yandoa isiyo na ulazima kuiepuka.mfano kama hupendi kitu fulani wewe baba ,huenda mkeo anakipenda basi hebu jaribu kuona nikwa nini mkeo anakipenda kitu hicho na mkazungumza nakuelewana,kuwa ikitokea mkeo anakifanya kitu hicho utakuwa una juwa hicho ndo humpa furaha,nk. nimuhimu sana kuwa nafuraha katika maisha yako.kaka s

ray njau said...

Ndoa ni ndoana ukiwa nayo na ni doa ukiipoteza.
[A house is made of bricks and stones but home is made 'malove' alone].