Thursday, February 2, 2012

Kweli pamoja tunaweza tukazuia hali hii isitokee katika nchi yetu?



Kw pamoja naamini tunaweza kufanya hali hii isitokee katika taifa letu ingawa kuna maeneo kuna hali ngumu ambao hata huwezi kuizungumza, ndugu zangu wazalendo tuungane pamoja bila kujali wewe ni chama gani, dini au ukabila tuseme sasa inatosha na hali hii.

5 comments:

ray njau said...

Hii ni hali halisi katika ncha zote za dunia na kamwe hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kubadili hali hii kutokana na ubinafsi wa mioyo ya wanadamu.
Hii ndiyo sababu wanadamu kila siku wanaendelea kusali ili wapate msaada kutoka kwa muumba wa mbingu, nchi na vyote vilivyomo.
-------------------------------
Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba :
“Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa duniani
kama huko mbinguni.
Utupatie leo riziki zetu za kila siku.
===================================

Yasinta Ngonyani said...

Hata kama hii ni hali halisi lakini kwa kugawana kili tulichonacho tunaweza tukaokoa kitu. Binadamu haturidhiki na kimoja nimeangalia hapo na nimepata elimu fulani ambayo inabidi niifanyie kazi.

Baraka Chibiriti said...

Tunaweza kabisa, ila ubinafsi tu ndo umezidi na kututawala kila kukicha....wewe angalia Tz majumba ya kifahari kila siku yanajengwa, unajiuliza wanapata wapi hela? Lakini jibu halipatikani, magari ya kifahari ndo usiseme......halafu tunasema sisi maskini, wanyonge wanazidi kuwa wanyonge kila siku.....lakini mimi siamini kabisa kuwa nchi yetu maskini.
Wito wangu kwa Wadau wote...kama unaweza kudhibiti hali kama hii isitokee...usisubiri Serikali au sijui nini, fanya kwa moyo wote malipo yako yapo tu, tena ni makubwa sana. Watu wengi husema; ningekuwa kiongozi ningesaidia, hata bila kuwa kiongozi, kama unaweza kusaidia....saidia ili hali iwe nzuri, uki mwokoa mtoto hata mmoja....ni thawabu kubwa sana.

simba deo said...

Ndiyo. Mtakumbuka kwamba 'Nabii Issa' alisema kwamba yatupasa kuzikana nafsi zetu. Ni kwa kupiga vita ubinafsi tu ndiyo tunaweza kujiletea ukombozi wa kweli. Ukweli utakuweka huru. Wengi wetu bado tunafikiri kwamba kwa kujilimbikizia mali nyingi ndivyo tunavyokuwa bora zaidi. La hasha ... kwa kufanya hivyo, ndivyo tunavyokuwa na 'utupu' katika maisha yetu. TUNAWEZA. Kila mmoja afanye sehemu yake kama inavyompasa. Tutabadilisha dunia nzima.

cytotec said...

obat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat telat bulan